Rais Samia, tafadhali usianzishe mchakato wa Katiba mpya mpaka ujiridhishe usimamizi wa mchakato huu

Rais Samia, tafadhali usianzishe mchakato wa Katiba mpya mpaka ujiridhishe usimamizi wa mchakato huu

..nadhani hizo amendments ndio zita-set the stage ya kuwa na mazingira rafiki na wezeshi ya kuandika katiba mpya.

..watu wametoka "GEREZANI" muda mfupi uliopita, kuna wengine bado wako "EDA," halafu unataka wakae pamoja waandike katiba mpya?
Unadhani itashindikana?

Bora tutengeneze mapema mazingira ya watu kutopelekwa tena "gerezani" siku za usoni kuliko kuchelewa maana hakuna ajuae kesho yake.
 
Uko sahihi katiba hii inahitaji some amendments baadhi ambazo ni mahitaji ya wakati huu kwa Sasa kama kuhusu tume ya uchaguzi, baadhi ya vitu ambavyo vimepitwa na wakati kwenye katiba yetu.
Kwahiyo hakuna haja ya katiba mpya??? Hizo kelele za wananchi wala zisitushughulishe??

Mama afanye tu amendment ya namna ambavyo tutaipata tume ya uchaguzi iliyo huru???

Kwa mfano hebu wewe tuambie ni namna gani tutaipata tume huru ya uchaguzi????
 
Kwahiyo hakuna haja ya katiba mpya??? Hizo kelele za wananchi wala zisitushughulishe??

Mama afanye tu amendment ya namna ambavyo tutaipata tume ya uchaguzi iliyo huru?
Katiba ni muhimu Ila hata hii ikianza kuboreshwa some part ambavyo ni mahitaji ya Sasa itapendeza, katiba itakayoruhusu matokeo ya uraisi kupingwa mahakamani, kuwa na tume huru isiyoegemea upande wa chama chochote, na hata Raisi kupunguziwa mamlaka ya teuzi kubwa wakurugrnzi mbalimbali ambao mwisho wa siku wanakuja ku save interest za bosi na sio interest za wananchi na katiba.

So it's possible to amend some parts of our constitution. Hii tabia ya wakurugenzi kupewa mamlaka ya kumtamganza yoyote ambaye hata hajashinda sio sawa loh.
 
Mchango murua huu.

Hapa nimepata mawazo kama ambavyo natamani iwe. Tuchangie kwa kujibu maswali ya msingi yaliyokuwepo kwenye mada.

Mkuu unasema tuanzie na rasimu ya Jaji Warioba na tuendelee mbele, hakuna haja ya kukusanya maoni mapya. Naamini hii ni ili kuokoa rasilimali muda na rasilimali fedha, au sio?...
Kwenye hiyo 80% ya wataalamu, nimemaanisha wale wadau waliobobea wa makundi mbalimbali katika jamii! Mfano Wafanyabiashara, Wajasiriamali, Madereva, Wakulima, Wafanyakazi, Walemavu, Diaspora, Wachumi, Viongozi wa dini, Wanahabari, Waajiri, Wamiliki wa Makampuni, Wamiliki wa taasisi za kifedha, nk

halafu na wanasiasa 20% pekee kutoka pande zote mbili za Muungano na pia vyama vyote Vikuu na vidogo vya siasa nchini. Naamini Bunge la aina hii litajadili mambo mengi yenye tija kuliko malumbano ya Serikali ipi inayofaa nchini. (Mbili - CCM) au (Tatu - UKAWA + Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba)
 
Katiba ni muhimu Ila hata hii ikianza kuboreshwa some part ambavyo ni mahitaji ya Sasa itapendeza, katiba itakayoruhusu matokeo ya uraisi kupingwa mahakamani, kuwa na tume huru isiyoegemea upande wa chama chochote, na hata Raisi kupunguziwa mamlaka ya teuzi kubwa wakurugrnzi mbalimbali ambao mwisho wa siku wanakuja ku save interest za bosi na sio interest za wananchi na katiba. So it's possible to amend some parts of our constitution. Hii tabia ya wakurugenzi kupewa mamlaka ya kumtamganza yoyote ambaye hata hajashinda sio sawa loh.
Nakubaliana na wewe mkuu. Lakini hujanjibu swali langu bado.

Na hapa ndio utathibitisha kwamba hili suala hatupaswi kulikurupukia tu.

Swali linarudi pale pale, ni namna gani tutapata tume huru ya uchaguzi???

Sisi ndio Great thinkers.
 
Kwenye hiyo 80% ya wataalamu, nimemaanisha wale wadau waliobobea wa makundi mbalimbali katika jamii! Mfano Wafanyabiashara, Wajasiriamali, Madereva, Wakulima, Wafanyakazi, Walemavu, Diaspora, Wachumi, Viongozi wa dini, Wanahabari, Waajiri, Wamiliki wa Makampuni, Wamiliki wa taasisi za kifedha, nk...
Sawa mkuu. Umeskika
 
Mchakato wa kutunga katiba mpya hugharimu muda mrefu na fedha nyingi mno, inahitaji kuwa ni mkakati wa kitaifa na agenda hiyo ibebwe na serikali kwani budget ya gharama za mchakato huo inabidi iwepo...
Anaweza kuwa na nia njema shida ni Msoga line, kumbuka mchakato ulivyoanza vizuri na timu ya Jaji Warioba, Msoga line na genge lake wakauharibu dakika za mwisho, kwahiyo hata this time mambo yanaweza kurudi yaleyale
 
Mimi nakubaliana kabisa na rasimu ya Warioba, na sio lazima tuwe na kundi kubwa la watu hasa wanasiasa, bali tuwe na watu wa makundi yote wasiozidi 100. Jaji Warioba awe ndio kiongozi wa tume hiyo, ashirikiane na Rais kuteua wajumbe, na mimi Tindo wa jf nikiwepo. Kitu pekee kwenye rasimu kinaweza kuondolewa, na ama kuwekwa vizuri ni uwepo wa serikali ngapi ndani ya muungano.

Kwa mara ya kwanza niliona tume iliyofanya kazi kizalendo tena iliyokuwa na wanaccm. Tume ile ya Jaji Warioba ilifanya kazi yake kwa weledi mkubwa, japo iliingiliwa na fitina za wanaccm. Ni bahati mbaya tu JK alikubali kazi ile nzuri ya tume kuharibiwa na itikadi za kisiasa hasa zikiongozwa na chama chake. Makundi yanayopaswa kutoa watu kwenye katiba hiyo.
Majaji 10
Wanajeshi 5
Polisi 2
Askari magereza 2
Uhamiaji 2
Viongozi wa dini 16
Wafugaji 5
Wakulima 5
Wafanyakazi 5
Wafanyabiashara 5
Wanasiasa 20. Uwiano wa vyama.
Viti maalum 30 ambao ni sisi watu wa mitandaoni, na wengine wenye ushawishi kwenye jamii , lakini wenye uelewa mpana wa mambo. Hapo tutapata katiba ya uhakika.
 
Kwa hiyo katiba mpya iwe ile ya Jaji Warioba?!!!

Naipinga katiba ile....

Katiba yetu ibaki na JMT yenye serikali mbili tu......

#KaziIendelee
 
Mkuu, with all due respect naomba nipingane nawe.

Waliopelekea mchakato kuharibika walikuwa ni UKAWA baada ya kuamua kutoka nje ya Bunge. Na sisemi kwamba walikosea, hapana!

Mimi nadhani walikuwa na hoja za msingi ambazo pengine Mama anazijua maana yeye likuwa kaimu mwenyekiti ambazo zilihitaji kufanyiwa kazi kwa maslahi mapana ya Watanzania.
 
Mimi nakubaliana kabisa na rasimu ya Warioba, na sio lazima tuwe na kundi kubwa la watu hasa wanasiasa, bali tuwe na watu wa makundi yote wasiozidi 100. Jaji Warioba awe ndio kiongozi wa tume hiyo, ashirikiane na Rais kuteua wajumbe, na mimi Tindo wa jf nikiwepo. Kitu pekee kwenye rasimu kinaweza kuondolewa, na ama kuwekwa vizuri ni uwepo wa serikali ngapi ndani ya muungano.

Kwa mara ya kwanza niliona tume iliyofanya kazi kizalendo tena iliyokuwa na wanaccm. Tume ile ya Jaji Warioba ilifanya kazi yake kwa weledi mkubwa, japo iliingiliwa na fitina za wanaccm. Ni bahati mbaya tu JK alikubali kazi ile nzuri ya tume kuharibiwa na itikadi za kisiasa hasa zikiongozwa na chama chake. Makundi yanayopaswa kutoa watu kwenye katiba hiyo.
Majaji 10
Wanajeshi 5
Polisi 2
Askari magereza 2
Uhamiaji 2
Viongozi wa dini 16
Wafugaji 5
Wakulima 5
Wafanyakazi 5
Wafanyabiashara 5
Wanasiasa 20. Uwiano wa vyama.
Viti maalum 30 ambao ni sisi watu wa mitandaoni, na wengine wenye ushawishi kwenye jamii , lakini wenye uelewa mpana wa mambo. Hapo tutapata katiba ya uhakika.
Inaonekana Watanzania karibu wote tuna msimamo mmoja juu ya kuanza upya au kuendelea na rasimu ya Jaji Warioba. Hili inawezekana lipo clear already.

Hapo kwenye hao watu wa kushiriki kwenye bunge la katiba sasa ndio balaa lipo hapo. Na ndio maana nkasema, Mheshimiwa Rais asiuanzishe mchakato huu mpaka apate watu wa kuaminika ambao hawatatutia hasara kama taifa kama ilivyotokea kipindi kile.

Huu mchakato ni mgumu sana jamani na kuthibitisha hilo, wengi wetu hatuwezi kuipanga safu ambayo inaweza ikaitwa bunge la katiba.

Leo nikikwambia mkuu tindo upendekeze majina ya watu ambao wanatakiwa wawepo katika hayo makundi uliyoyataja naamini hutoweza. Kwa mfano, pendekeza hao polisi wawili, askari magereza wawili, uhamiaji wawili viongozi wa dini 16 wafugaji watano wakulima watano (huku ukijua Sumry nae na mkulima 😀 😀 😀 😀 )

Hao wanasiasa 20 mkuu utazua balaa kubwa hapo na majina utashindwa kuja nayo.

Kiufupi hao watu mia wakichaguliwa basi yatazuka makubwa kwamba katiba ni ya hao watu 100 na sio ya Watanzania.

Kwenye wanamichezo tafadhali ndugu yangu isajorsergio asikose.
 
Kwa hiyo katiba mpya iwe ile ya Jaji Warioba?!!!

Naipinga katiba ile....

Katiba yetu ibaki na JMT yenye serikali mbili tu......

#KaziIendelee
Ile ni rasimu tu mkuu, kwanini unaipinga?

Kwa hiyo unapendekeza mama aanze upya?

Mimi napingana na wewe kwenye katiba ya serikali mbili mkuu.
 
Ile ni rasimu tu mkuu, kwanini unaipinga?

Kwa hiyo unapendekeza mama aanze upya?

Mimi napingana na wewe kwenye katiba ya serikali mbili mkuu.
Sawa mkuu wangu nimeridhia unipinge.....👍

Mkuu unaihitaji katiba ya serikali tatu?!!!

TANGANYIKA tuliyoizika 6 feet under the ground IFANYIWE maombi na dua ifufuliwe mkuu?!!!!
 
Rasimu ya Jaji Warioba hiyo hatua ilishapita. Hatua iliyopo ni Katiba pendekezwa kupelekwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni.
Tuanze afresh au tukaipigie kura Katiba pendekezwa. Kurudi kwenye hatua iliyokwisha pita ni unconstitutional kwa maoni yangu.
 
Back
Top Bottom