Rais Samia: Tanzania inayo nafasi ya kuuza umeme nje

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wakuu

Rais Samia akiongea kwenye Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika leo Januari 28,2025 Jijini Dar es salaam.

"Tanzania ni moja ya Nchi 12 zitakazozindua mpango mahususi wa kitaifa kuhusu nishati, kupitia mpango wetu tunatarajia kuongeza kasi ya kuunganisha umeme nchini hadi kufikia 72% ifikapo mwaka 2030, ili kufanikisha azma hiyo ndani ya muda wa miaka mitano ijayo, tutahitaji uwekezaji wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 13, ambapo dola bilioni 5 zitapatikana kutoka sekta binafsi hapa nchini."

"Kupitia mpango huu tumepanga kuongeza uzalishaji wa umeme kutokana na nishati mchanganyiko, Tanzania ni kiungo muhimu katika kuunganisha umeme Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika na hivyo kuwezesha biashara ya umeme kutoka Afrika Kusini hadi Misri, tayari tumeunganisha miundombinu ya umeme na Nchi za Burundi, Kenya na Rwanda na sasa tunaendelea kuunganisha miundombinu ya umeme na Nchi ya Zambia na Uganda"

"Kuwepo kwa miundombinu hiyo kutawezesha biashara ya nishati kati ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC, Tanzania inayo nafasi ya kuuza umeme ikizingatiwa kuwa hadi November 2024 mahitaji ya umeme Tanzania yalikuwa megawatt 1888 wakati uzalishaji wetu mi megawatt 3431"

"Muelekeo wetu ni kufikisha umeme katika vitongoji vyote 64359 baada ya kufanikiwa katika vijiji vyote vya Tanzania, hadi sasa tumevifikia vitongoji 32827 na kazi inaendelea katika vitongoji vilivyobakia, la nne ambalo mpango huu utafanya ni kusambaza nishati safi ya kupikia"

Soma: Rais Samia akizungumza katika Africa Head of State Energy Summit (mission 300), January 28th, 2025
IMG_2831.jpeg
 
Madhara ya "speech" za kuandikiwa, alafu mwandishi mwenyewe ni Aina ya akina Januari Makamba, na msomaji ni........
 
Huu huu unao waka kama POWER BANK?
KAZI ni kipimo cha UTU
 
Wakuu

Rais Samia akiongea kwenye Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika leo Januari 28,2025 Jijini Dar es salaam.

"Tanzania ni moja ya Nchi 12 zitakazozindua mpango mahususi wa kitaifa kuhusu nishati, kupitia mpango wetu tunatarajia kuongeza kasi ya kuunganisha umeme nchini hadi kufikia 72% ifikapo mwaka 2030, ili kufanikisha azma hiyo ndani ya muda wa miaka mitano ijayo, tutahitaji uwekezaji wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 13, ambapo dola bilioni 5 zitapatikana kutoka sekta binafsi hapa nchini."

"Kupitia mpango huu tumepanga kuongeza uzalishaji wa umeme kutokana na nishati mchanganyiko, Tanzania ni kiungo muhimu katika kuunganisha umeme Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika na hivyo kuwezesha biashara ya umeme kutoka Afrika Kusini hadi Misri, tayari tumeunganisha miundombinu ya umeme na Nchi za Burundi, Kenya na Rwanda na sasa tunaendelea kuunganisha miundombinu ya umeme na Nchi ya Zambia na Uganda"

"Kuwepo kwa miundombinu hiyo kutawezesha biashara ya nishati kati ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC, Tanzania inayo nafasi ya kuuza umeme ikizingatiwa kuwa hadi November 2024 mahitaji ya umeme Tanzania yalikuwa megawatt 1888 wakati uzalishaji wetu mi megawatt 3431"

"Muelekeo wetu ni kufikisha umeme katika vitongoji vyote 64359 baada ya kufanikiwa katika vijiji vyote vya Tanzania, hadi sasa tumevifikia vitongoji 32827 na kazi inaendelea katika vitongoji vilivyobakia, la nne ambalo mpango huu utafanya ni kusambaza nishati safi ya kupikia"

Soma: Rais Samia akizungumza katika Africa Head of State Energy Summit (mission 300), January 28th, 2025
View attachment 3216508
Good narration... Kongole Madam Prezdaa
 
Hii nchi Hata Hawa wanangu wadogo wakipunguza michezo wanaweza kuiongoza

Samia anatupa ahadi za 2030 ambazo hazitekelezeki anajua atakua kashasepa na hakuna wa kumfanya kitu
 
Ukweli ni kuwa hatuna umeme wa kuuza. MW 3500 tunaona nyingi sana wakati nchi kama Misri wana MW zaidi ya 40,000 huko. South wako huko 60,000. Pia zaidi ya asilimia 50 ya watu hawana umeme. Bado sana sisi. Tuongeze uzalishaji na kuunganisha watu kwa umeme. Walau tufike MW 10,000 ndiyo tuanze kuongea kuuza umeme.
 
kumbe umeme tunao!!
Kwahiyo hii katakata wanatufanyia makusudi?
 
Back
Top Bottom