Rais Samia: Tanzania inayo nafasi ya kuuza umeme nje

Ukweli ni kuwa hatuna umeme wa kuuza. MW 3500 tunaona nyingi sana wakati nchi kama Misri wana MW zaidi ya 40,000 huko. South wako huko 60,000. Pia zaidi ya asilimia 50 ya watu hawana umeme. Bado sana sisi. Tuongeze uzalishaji na kuunganisha watu kwa umeme. Walau tufike MW 10,000 ndiyo tuanze kuongea kuuza umeme.
kwani hata wakiuza hiyo pesa inaingia mifukoni kwa majizi waliokuwa wanakula songas na IPTL..ukisoma hiyo hotuba ya rais mahitaji ya nchi kwa sasa ni megawat 1888 na umeme uliopo kwenye mfumo ni megawat 3500.. kwahiyo mifumo ya kusafirisha umeme wanayojenga kuelekea nchi mbalimbali lengo ni kuuza hiyo ziada baada ya kutoa mahitaji ya nchi na usikute hata hiyo megawat 1888 wanaimega pia kujazia kwenye mauzo yao ndiomaana shida za umeme haziishi nchini kumbe kuna wahuni wanafanya biashara mpaka kile kidogo kinachobaki kama megawat 1200 tunajitutumua kuuza ni tamaa iliyoje..ila wenzetu wana mpaka MW 40,000-60,000 wametulia tu..JPM kapambana mno kujenga lile bwawa alafu mafisi wanakula mavuno kiulaini kivulini badala ya kupunguza ukali kwa wanachi inatia hasira sana.!
 
Wakuu

Rais Samia akiongea kwenye Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika leo Januari 28,2025 Jijini Dar es salaam.

"Tanzania ni moja ya Nchi 12 zitakazozindua mpango mahususi wa kitaifa kuhusu nishati, kupitia mpango wetu tunatarajia kuongeza kasi ya kuunganisha umeme nchini hadi kufikia 72% ifikapo mwaka 2030, ili kufanikisha azma hiyo ndani ya muda wa miaka mitano ijayo, tutahitaji uwekezaji wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 13, ambapo dola bilioni 5 zitapatikana kutoka sekta binafsi hapa nchini."

"Kupitia mpango huu tumepanga kuongeza uzalishaji wa umeme kutokana na nishati mchanganyiko, Tanzania ni kiungo muhimu katika kuunganisha umeme Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika na hivyo kuwezesha biashara ya umeme kutoka Afrika Kusini hadi Misri, tayari tumeunganisha miundombinu ya umeme na Nchi za Burundi, Kenya na Rwanda na sasa tunaendelea kuunganisha miundombinu ya umeme na Nchi ya Zambia na Uganda"

"Kuwepo kwa miundombinu hiyo kutawezesha biashara ya nishati kati ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC, Tanzania inayo nafasi ya kuuza umeme ikizingatiwa kuwa hadi November 2024 mahitaji ya umeme Tanzania yalikuwa megawatt 1888 wakati uzalishaji wetu mi megawatt 3431"

"Muelekeo wetu ni kufikisha umeme katika vitongoji vyote 64359 baada ya kufanikiwa katika vijiji vyote vya Tanzania, hadi sasa tumevifikia vitongoji 32827 na kazi inaendelea katika vitongoji vilivyobakia, la nne ambalo mpango huu utafanya ni kusambaza nishati safi ya kupikia"

Soma: Rais Samia akizungumza katika Africa Head of State Energy Summit (mission 300), January 28th, 2025
View attachment 3216508
 
Attachments

  • IMG-20250309-WA0067.jpg
    IMG-20250309-WA0067.jpg
    72.3 KB · Views: 1
Someone should tell her, the main issue is not to collect money but to ensure that electricity is available and affordable..., nadhani we are missing the plot big time....

Kupata wawekezaji na watu binafsi ni kuongeza watu kati wa kugawana faida hivyo bei lazima ipande bei (after all kila mtumiaji pesa yake imeshachotwa sana na kina REA as well as kulipa madeni ya Uwekezaji)

Pili how does it make sense tuuze umeme nje ili tupate pesa ili tununue LPG nje ili tuje tupikie wakati tungefanya umeme ukawa afforadble wala tusingehitaji kununua LPG, ofcourse kwa vyanzo tulivyo navyo tungeweza pia kuuza nje...

Ila ndio hivyo tunapoteza nafasi hio kwa kuuza crown jewels za taifa
 
Wakuu

Rais Samia akiongea kwenye Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika leo Januari 28,2025 Jijini Dar es salaam.

"Tanzania ni moja ya Nchi 12 zitakazozindua mpango mahususi wa kitaifa kuhusu nishati, kupitia mpango wetu tunatarajia kuongeza kasi ya kuunganisha umeme nchini hadi kufikia 72% ifikapo mwaka 2030, ili kufanikisha azma hiyo ndani ya muda wa miaka mitano ijayo, tutahitaji uwekezaji wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 13, ambapo dola bilioni 5 zitapatikana kutoka sekta binafsi hapa nchini."

"Kupitia mpango huu tumepanga kuongeza uzalishaji wa umeme kutokana na nishati mchanganyiko, Tanzania ni kiungo muhimu katika kuunganisha umeme Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika na hivyo kuwezesha biashara ya umeme kutoka Afrika Kusini hadi Misri, tayari tumeunganisha miundombinu ya umeme na Nchi za Burundi, Kenya na Rwanda na sasa tunaendelea kuunganisha miundombinu ya umeme na Nchi ya Zambia na Uganda"

"Kuwepo kwa miundombinu hiyo kutawezesha biashara ya nishati kati ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC, Tanzania inayo nafasi ya kuuza umeme ikizingatiwa kuwa hadi November 2024 mahitaji ya umeme Tanzania yalikuwa megawatt 1888 wakati uzalishaji wetu mi megawatt 3431"

"Muelekeo wetu ni kufikisha umeme katika vitongoji vyote 64359 baada ya kufanikiwa katika vijiji vyote vya Tanzania, hadi sasa tumevifikia vitongoji 32827 na kazi inaendelea katika vitongoji vilivyobakia, la nne ambalo mpango huu utafanya ni kusambaza nishati safi ya kupikia"

Soma: Rais Samia akizungumza katika Africa Head of State Energy Summit (mission 300), January 28th, 2025
View attachment 3216508
Kwanza kabisa nipende kumshukuru mama kwa kuuza umeme nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom