Rais Samia: Tanzania kuchora ramani yake mpya

Usijali, nyie huko unyumbuni si mnaongozwa na lissu na heche....basi jifarijini nao huku mkitupia tone tone za hapa na pale.
Uzuri kuwa wametaka wenyewe kuliwa kwa hiyo tuwaache wacharazwe kweli kweli, wajinga ndio waliwao tone tone hoyeee.
 
Kama ni kweli au watu anataka reaction mimi nashauri asifanye hivyo ila kama anajiamini afanye ila ahakikishe anaweza asije ishia njiani nakutuacha na maswali magumu... kuna vitu sio vya kugusa maana vipo chini ya jamuhuri wala sio Rais wala havitaki siasa End.
 
wasisahau eneo la kipande cha znz kilichopo bagamoyo kuki highlight kama eneo la znz!, inhependeza nasi bara tukawa na eneo znz likawa highlighted kama Tanganyika, kwa hili tutakuwa tumeuweka muungano wetu supa glue!
#Intelegency imenituma hayo!
 
Bilioni 133, mradi wa mabasi yaendayo kasi Mbagala bado mchakato unaendelea.
Lkn hapa nimekumbuka msemo usemao Mshika mbili moja humponyoka, watu wa Mbagala subirini uchaguzi ukaribie tutakuja kuzindua. Any way naelekea airport kupokea ndege mpya
 
Usije ukakuta anafikiria kutoa kipande cha ardhi ya Tanzania kwa Wamalawi kupitia ziwa Nyasa, atakuwa ametenda kosa kubwa mno yeye kama Mzanzibari!
 
Kweli kila shughuli ni pesa.
Sasa kama nia ya dhati ipo , wapime miji yote kuondoa makazi(makazi holela yasiyo kuwa na barabara yasiyozingatia utaratibu wa mipango miji).

Kabla ya kuongeza maeneo mapya ya utawala kwa nini upimaji haufanyiki?!
Miaka 60 bado tunapima tu ardhi serious?
 
Mikataba hiyo iliyowekwa na wakoloni lazima tuiheshimu. Vinginvyo unaonaje Kenya wakadai sehemu za Kilimanjaro, au Serengeti ni zao? Kumbuka hata ziwa Nyanza halimilikiwi kwa usawa kati ya Tanzania, Kenya na Uganda.
 
Sawa itaonyesha mikoa na wilaya zilizoongezeka. Lakini gharama za uchoraji sasa billion ngapi? 🤔🤔🤔
Ushaanza kuchorwa ni magu era na watu tumekutana nao wakiwa site sa sijui ndo Ile au tunaanza moja
 
ramani ya mwisho ya Tanzania, ilichorwa mwaka 1978, kwa kiasi kikubwa kuna mabadiliko makubwa hata ukichua tu, Jiji la Dar es Salaam, la mwaka 1978 na leo


Hii ramani naona ina mikoa mipya ya
Geita
Simiyu
Katavi
Songwe
Njombe
Je iligawanywa 1978 au nani ameichora ramani hii?
 
Rais samia ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Ardhi ya Mwaka 1995 (Toleo la 2023) uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre (JKCC) - Dodoma.
Hii ndiyo ile wamesema inawafavour wageni
 
Ziwa Nyasa mpaka wa Tanzania utakuwa katikati au ufukwe wa mashariki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…