Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suhulu Hassan amesema kuwa Tanzania ni nchi ambayo Mwenyezi Mungu ameibariki neema nyingi sana.
Amesema hayo wakati akitoa hotuba yake kwenye hafla ya maadhimisho ya miaka 50 ya WAWATA (Wanawake Wakatoliki Tanzania) iliyofanyika uwanja wa Benjamin Mkapa, Septemba 11, 2022.
“……Tanzania ni nchi nzuri. Tuna mambo mengi ya kujivunia, tunaweza kufanya biashara popote kupitia bandari ya Dar es salaam, tuna maziwa, mito na ardhi yenye rutuba kubwa. Tuna madini ambayo mengine hata hatujui majina yake. Tatizo ni namna gani ya kutumia” amesema Rais.
Rais amesema kuwa anayo matumaini makubwa kuwa kadri muda unavyokwenda, Tanzania itaweza kujisimamia vizuri pamoja na kuzitumia rasilimali hizi kwa ufanisi na manufaa makubwa kwa nchi.