"Tatizo ni namna ya kuyatumia"
Hiyo kauli nayo ni tatizo, kwamba Rais anamaanisha Mungu ametupa "wajinga" madini ambayo hatujui namna ya kuyatumia ili kuliondoa hili taifa kwenye lindi la umaskini?
Nyerere aliwahi kutoa kauli inayofanana na hiyo miaka mingi iliyopita, akiwaasa wenzie huko CCM wayaache hayo madini mengi ardhini mpaka pale watanzania wakiwa na uwezo wa kuyachimba wenyewe, akapuuzwa.
Lakini, kauli kama hiyo inaporudiwa leo, zaidi ya miaka thelathini baadae inaonesha tatizo sio ujinga wa watanzania, bali tatizo ni ujinga wa viongozi wa CCM, hawa ni wabinafsi na walafi, muda wote wanawaza 10%.
Ndio maana wanasababisha taifa lisione faida ya kuwa na madini licha ya kuwa na wasomi wengi kuliko wakati ule Nyerere alipoitoa hiyo kauli kwa mara ya kwanza.
Sasa namshauri Rais wetu afuate ule ushauri wa Nyerere alioutoa miaka ile, kwamba, viongozi wa serikali ya CCM wayaache hayo madini yabaki ardhini mpaka pale ujinga wao utakapoondoka kwenye vichwa vyao, ili wasizidi kulitia hasara taifa.