Rais Samia: Tanzania tuna madini mengi kiasi ambacho mengine hatujui yanaitwaje

hahahahaha kuwa madini ni suala lingine na kuyachimba ni suala nyingine.

Hakuna jambo zuri na muhimu kama taifa kuwa na watu wakutosha wenye maarifa yakutosha.
 
Yawezekana kuna uhusiano hasi kati ya akili na madini. Nchi nyingi zenye madini hazina akili za kunufaika na hayo madini.Mwisho tunaishia kujiita matajiri lakini mfukoni teee!
Yani mfukoni mbongo teee, ni kukamuana tozo tu,
 
Hili nalo mkalitizame
 
"Neema ambayo MUNGU ameumba hapa duniani... Tuyatumie maumbile haya kwa maendeleo yetu.. Asanteni sana kwa kunisikiliza.. Kristuuuuu.. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania... Asanteni sana WAWATA.."

In SSH Voice
 
Si wayaite tozonia!
Au mengine ndio yale yenye majina ya mwigulu nchemba rais 2015?
Mbona majina ni mengi tu.

Waache kutukata tozo!

Tozo ni wizi!
 
Mtangulizi wake alikuwa anayajua yote na mahali yalipo na thamani yake. Ye kama hajui basi hatoshi.
 
Wenzetu Botswana wana uzoefu kwenye masuala ya madini na wameendelea kwa kutumia rasilimali hiyo.

Pia SADC ipo, hivyo twahitaji ushirikiano tu.

Tatizo la baadhi yetu sisi waafrika kujiona twafahamu kila kitu kumbe tupo nyuma sana kwenye tasnia ya kufikiri kwa undani.
 
Kwa miaka 60 hatujatumia rasilimali zetu kutuondolea umaskini .
tatizo watawala siku zote hutumia nguvu nyingi kupambana na vyama vya upinzani, na wanaharakati wenye mawazo na sera mbadala.
 
Tatizo letu watanzania ujuaji na uvivu umekithiri sana. Hii kasumba kama hatutaiacha basi kizazi chetu kitabakia nyuma Kwa Karne ijayo. Mh Rais amemaanisha kuwa Sisi tu matajiri na utajiri wetu tunaweza kunufaika nao kupitia masoko yaliyopo nk. Tozo ni lazima tutoe na labda jambo la muhimu hapo ni kutizamwa upya viwango ukizingatia na Hali halisi ya maisha ya watanzania Kwa Sasa. Mama yetu anapambana kuhakikisha nchi inapona majeraha ya mdororo wa uchumi duniani Sisi tumekalia makelele tu.
 
Hapo kimeelewa tu maumbile yetu tuliyojaliwa na mwenyezi Mungu tuyatumie kwa maendeleo yetu
 
Nadhani madini ya tozo ndiyo mengi zaidi,tuendelee kuyachimba tu.
 
Ipo siku atakuja mtawala atasema madini yote yameisha.
Hapo ndipo tutakapoelewa siasa ni kitu gani.
Machimbo mengi ya dhahabu yanavumbuliwa na wachimbaji wadogo. Baada ya muda anapewa mwekezaji feki, anakopea hela anafanyia mambo yake, migodi inasimama haindelezwi na mrabaha hakuna. Mwisho tutaambiwa madini yametoweka
 
Tuna madini mengi lakini tunategemea tozo
 
Nakuunga mkono kwa [emoji817]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…