#COVID19 Rais Samia: Tanzania tuna wagonjwa wa Wimbi la Tatu la Corona

Hebu jaribu hata kidogo kuficha upumbavu wako, unataka hadi wewe uugue au umzike mkeo kwa Corona ndo ujue ipo?



Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Hebu jaribu hata kidogo kuficha upumbavu wako, unataka hadi wewe uugue au umzike mkeo kwa Corona ndo ujue ipo?



Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
Mkuu Kuna Jambo nimetoka kupost muda si mrefu. Mama Samia anasema corona ipo na tuchukue tahadhari ila jana yeye kapiga simu na kumpongeza nandy akiwa live jukwaani kwenye Nandy festival. Watu walikuwa wengi wamebanana hatari hakuna cha barakoa wala nini. Nilitegemea angechukizwa na hiko kitendo na kuwawajibishwa walioruhusu hiyo show kwenye kipindi Kama hiki wimbi la tatu
Tusubiri
 
TUNAWAMBIA KILA SIKU,nyakat zimekwisha, muda wa dunia umefika mwsho, tuko ktk nyakat mbaya na zakutisha kulko nyakat zozote tangu dunia iumbwe, kwa bahat mbaya kuna mambo tuliyofundishwa kuwa kwel kumbe ni ya uongo, tunaish ktk uongo, tunakula uongo, tunajifunza uongo, tunaabudu uongo, na kupewa tawala znazotawala kwa uongo kupitia baba yao wa uongo ibilisi, hii dunia kwa ilpofika ni lazma wakuu wa nchi wafanye juu chin kutimiza kwa haraka zile ajenda za kuifanya dunia chini ya mamlaka moja, and soon yataibuka mambo mazito na yakutisha ambayo hata wale wanaopenda kutupinga wasomi, na kukutukana watatuamn, unafika ule muda ambao viongoz wetu tunaowaamn watashirikiana kutuzamisha ktk kiza kinene uki wao wakineemeka na uongo wa yule bwana mkubwa wa uzunguni,,,tulipo ni pabaya na tunakoelekea ni afadhar wale waliokufa kulko ssi ambao tuko hai maana kuna majanga yatakayoikumba hii dunia na kwa akili za wabongo kuyamudu si rahis, viongoz wetu wa dini wanatusariti na wataendelea kutusariti, na ipo siku wataungana viongoz wote wa dini wataunganish dola ya serkali na dini vi operate pamoja kuwashinikiza raia kufanya kile serkal inataka,.na ndipo tulpo sasa, na ndpo dunia ilipo sasa, siongei haya mambo kwa kubahatisha ama kiuchochezi, bal ni ukwel harisi ambao lazma utokee na unatokea, wale wabishi na wanaopenda kunitukana freshi tu ipo siku mtaelewa nn kipo nyuma ya pazia ktk hiz serkal zetu znazotupofusha kwa makusudi...
 
JPM was right. Ni ninyi wenye akili finyu hamkuwa mnamwelewa yule shujaa. Alikuwa mtu aliyejaa Iman kwa Mungu muumba ambaye hashindwi chochote. Corona ni nini mbele zake?.
Kumbe. Kwa hiyo TZ nchi ya pekee yenye imani katika Mungu?? Au Mungu amesahau kidogo hivyo siku hizi anaelewa Kiswahili pekee?? Kama ni hivyo: kwa nini Wakenya (walioomba kwa Kiswahili wasiangamizwe Corona) walianza kufa? Au je Mungu amebadilisha mfumo wa kupokea maombi hasikii tena kama hayaletwi na mkuu wa nchi??
 
m napenda kuona koment za watu wenye msimamo kama ninyi, sio yale majinga yanakubar kila kitu, mm hata kwenye page ya rais samia huko twitter huwez kuta nasifia upumbv, bali uwaga natoa facts zenye msimamo ambapo kama rais angekuwa anazisoma basi yale mambo yote wanayo yatenda yakipuuz wangeachnan nayo
 
Kaka kama ni imani yako, basi iwe hivyo. Menginevyo hakuna dalili kwamba siku hizi ni mbaya kuliko nyakati za nyuma. Nikifungua macho naona mengi ya kinyume. Njaa imepungua kote duniani. Watu wanafikia umri mkubwa, idadi ya watoto wadogo wanaokufa imepungua sana shauri za chanjo. Naona baraka nyingi, pamoja na changamoto mpya, kama uharibifu wa mazingira asilia na machafuko ya hewa.
 
Mama anafeli sana, anyway, zigo ni lake, akisema tusiende kazini sisi poa, lockdown itakua ya kutokwenda kazini tu maana mitaani nina uhakika uswahilini maisha yataendelea, itakua likizo kwetu ya kazini.
Nani anasema lockdown? Watu wasipotenda kipumbavu hakuna haja katika mazingira ya hapa; kwa hiyo wakivaa barakoa, wakiepukana kubanana kwa kukaa karibu mno, pia kutunza usafi wa mikono - tayari athira inapungua sana. Kwa bahati nzuri watu wengi Dar es Salaam hawaishi katika nyumba penye madirisha ya kufunga kabisa, hivyo mabadiliko ya hewa yapo muda wote hali inayopunguza maambukizi.
 
Yule ndio amefanya watu wasiwe waoga wa corona......
sema akili fupi kama yako huwezi elewa
Hakika. Watu wanadunda tu mitaani bila hofu wala mabarakoa kwa sababu Magufuli aliwafungua akili.

Hata hawa wahuni wanaomtukana mitandaoni, hawavai mabarakoa kwa sababu walifunguliwa akili pia na chuma JPM.

Wanarelax na kujamba — Hakuna cha sanitaiza wala nini. Wamejiachia kwa raha zao.

Wanamtukana na kufyonya huku moyoni wanasema yesssss JPM is jembe.
 
Acha maneno maneno wewe!

Hizi janja janja za kitapeli tumeshazibaini.

Haiwezekani ugonjwa uwe kwenye matelevisheni tu na magazeti.

Janja janja za kitapeli hazina nafasi kwa sasa.

Hayo machanjo yenye sumu mkajidunge na baba zenu. Never ever ever.

Na msijaribu!
 
Dah... Xaxa hii ni atareee xana xana [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2960]
 
Kwa hiyo wewe umeona sehemu za kusitisha mikusanyiko ni Makanisa tu? Pumbavu kweli.
 
Punguza jazba. Kwanza ugonjwa huo haupo magazetini. Umo mwilini mwa watu. Umeshaua wengi. Rais alitembelea hospitali ambako daktari alimwonyesha wagonjwa wa Covid.
Hayo machanjo yameanza kuokoa maisha ya watu wengi. Katika nchi nyingi wanafanya juhudi kubwa kuwafikia watu wengi iwezekanavyo, tena kwa gharama kubwa.
Unaamini kweli dunia inajaa wajinga? Au wanacheza tu?
Pale ambako wengi wameshapata chanjo, maambukizi yamepungua tayari.

Binafsi nashukuru nimeweza kupata chanjo nilipotembelea nchi jirani.
Hiyo lugha ya chanjo sumu ni kitoto. Amka, kaka, washa bongo.
 
Kwamba Rais hakuwa na taarifa kwamba kuna wagonjwa wa corona pale hospitalini kabla hata ya kwenda ila amekuja kujua baada ya kwenda mwenyewe? yeye kaambiwa ni wagonjwa wenye matatizo ya kupumua ila yeye anasema covid na ndio akajibiwa hivyo hivyo covid, sasa sijui matatizo kupumua yote ni covid tu.
 

Kusitisha ibada kisa corona ni ukengeufu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…