#COVID19 Rais Samia: Tanzania tuna wagonjwa wa Wimbi la Tatu la Corona

Binadamu wengi sana pato lao hutegemea mikusanyiko. Wazungu wanaufahamu ukweli huo na wanakesha maabara wakitengeneza chanjo, wanataka maisha yarudi hali ile ya zamani.

Kuna matatizo makubwa kiakili yanayokwenda pamoja na maisha ya kujitenga. Kujiua kumeongezeka Ulaya na Marekani kipindi hiki cha corona.
Lakini sasa huku kwetu maisha yalisharudi kama zamani toka kitambo na wengine wanaamini barakoa ndio kinga kwenye hiyo mikusanyiko sasa sijui kwanini huko Ulaya na America hawakufanya kama sisi kutegemea barakoa tu na kuendelea na mikusanyiko.
 
Mama anafeli sana, anyway, zigo ni lake, akisema tusiende kazini sisi poa, lockdown itakua ya kutokwenda kazini tu maana mitaani nina uhakika uswahilini maisha yataendelea, itakua likizo kwetu ya kazini.
Akitangaza level seat kwenye daladala watu wanakaa chini wanajificha traffic haoni kama ile mwanzo.
 
Kwahio wewe unatakaje?serikali ndio imeshatangaza sasa kwamba kuna wagonjwa wa wimbi la tatu,kila mtu achukue tahadhari,kama unabisha endelea kubisha
Kutumia akili ni hatua ya kuonyesha wewe ni mtu wa aina gani na kutumia akili ya mtu mwingine unaonekana mtu wa aina gani, so decision is your!.

Kile anachokifanya Museveni au Kagame dhidi ya hicho unachosema "serikali ndio imeshatangaza sasa kwamba kuna wagonjwa..." ni tofauti na kabisa na maamuzi yenu.
 
BE WARNED

Stay at Home

From: A DOCTORS' GROUP KMA

Tafsiri ya haraka na Isaac Mruma.

UNAONYWA

Baki Nyumbani

KUTOKA KWA: MADAKTARI

Kirusi kimerudi, na wakati huu kimekuja na nguvu zaidi, mbinu za ziada na kwa kificho.

Hatukohoi, hakuna homa: ni maumivu tu ya viungo, kuishiwa nguvu, kupoteza hamu ya chakula na homa ya mapafu (nimonia) ya UVIKO (COVID)!
Kiukweli, idadi ya wanaofariki ni kubwa zaidi; ina chukua muda mfumo zaidi ugonjwa kufikia hali mbaya.
Wakati mwingine hakuna dalili za ugonjwa.. tuwe makini.

Hii ya sasa haijitokezi kwenye sehemu za pua na koo!
Inaathiri mapafu, hivyo inachukua muda mfupi zaidi.

Kuna wagonjwa kadhaa wasio na homa; lakini taarifa za X-ray zinaonyesha wana nimonia ya kifua!
Kipimo cha kupitia puani hakionyeshi UVIKO 19 (COVID 19)!

Hii inaonyesha kirusi kina kwenda moja kwa moja kwenye mapafu. Ndio maana hiki cha sasa ni hatari na kinaua zaidi.

Kuwa makini na epuka sehemu zenye mikusanyiko; vaa Barakoa, Nawa mikono yako mara kwa mara.

WIMBI hili la kirusi ni la hatari kuliko la kwanza na la pili. Hivyo tunawajibika kuwa makini sana na kuchukua tahadhari zote.

Sambaza ujumbe huu kwa watu wengi iwezekanavyo, kwa marafiki na Familia.

Tafadhali chukua tahadhari na uwe salama!

Copied from another group
 
Hivi hiyo hatari ni hatari kwa kiwango gani? maana toka wimbi la kwanza hadi la pili ila hatujaona huduma zetu za afya kuzidiwa kutokana na wagonjwa au kuzidi kwa wingi wa vifo kama tulivyosikia huko kwengine sehemu za kuhifadhi maiti kujaa na wengine kuni za kuchomana kuisha.
 
Hilo wimbi la tatu liko kwenye magazeti na televisheni, lakini huku mtaani hakuna cha wimbi wala bibi yake na wimbi.

Hizo fedha za wazungu mlizokula hakika mtazitapika majizi nyinyi. Maana hamuishi kuweweseka na makorona kama visungura tope.

Huku Buzza kwanza hatujui hata maana ya corona. Tunaisikiaga tu kwenye mitandao na majarida.

Kwendeni huko na mabarakoa yenu uchwara!

Matapeli wakubwa!

Sasa ndo mpka useme Buza, kumekukosea nini huko Buza
 
Unataka kuwabishia hata walio jikoni wanaona hali halisi ya ugonjwa unavyopukutisha uhai wa Watanzania?

Hivi hiyo hatari ni hatari kwa kiwango gani? maana toka wimbi la kwanza hadi la pili ila hatujaona huduma zetu za afya kuzidiwa kutokana na wagonjwa au kuzidi kwa wingi wa vifo kama tulivyosikia huko kwengine sehemu za kuhifadhi maiti kujaa na wengine kuni za kuchomana kuisha.
 
Mama anatakiwa awambie china watoe ushirikiano kwenye tafiti huru za chanzo cha hivi virusi. Bila kujua chanzo huu ugonjwa utatumaliza.
mi sijawahi sikia ugonjwa una awamu, ikifika 100 wave kuna mtu atakuwa amebaki kweli?
 
Hilo wimbi la tatu liko kwenye magazeti na televisheni, lakini huku mtaani hakuna cha wimbi wala bibi yake na wimbi.

Hizo fedha za wazungu mlizokula hakika mtazitapika majizi nyinyi. Maana hamuishi kuweweseka na makorona kama visungura tope.

Huku Buzza kwanza hatujui hata maana ya corona. Tunaisikiaga tu kwenye mitandao na majarida.

Kwendeni huko na mabarakoa yenu uchwara!

Matapeli wakubwa!
Takwimu zikianza kutolewa tutakimbiana...
 
Unataka kuwabishia hata walio jikoni wanaona hali halisi ya ugonjwa unavyopukutisha uhai wa Watanzania?
Sijabisha nimehoji tu sidhani kama ni vibaya kuhoji, corona ni ugonjwa hatari hilo linajulikana ndio maana nikatoa hiyo mifano ya wenzetu tunasikia huduma za afya kuzidiwa na hadi sehemu za kuhifadhi maiti pia kuzidiwa na hayo ni mambo ambayo yapo wazi hayahitaji mtu wa aliyeko jikoni kukwambia hizo athari za hatari ya corona ila sasa sisi bado corona yetu hatari yake wanaijua watu waliyoko jikoni tu.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Ndiyo sababu hao walioko jikoni kutokana na hali halisi wanayoiona huko jikoni wameamua kutoa tahadhari ili tuwe makini zaidi katika kupambana na hili gonjwa.

Hili la mama kwenda hospital bila ya interijensia yake kumpa full coverage ya eneo husika naona ni mazingaombwe tu.

Hivi ni kweli mama alikuwa hana taarifa za kina juu ya hospital hiyo kabla ya kwenda?

Eti nae anafika ndio anashtukizwa wagonjwa wa corona wapo. Ngoja nichekeko hahahaha
 
Mama anafeli sana, anyway, zigo ni lake, akisema tusiende kazini sisi poa, lockdown itakua ya kutokwenda kazini tu maana mitaani nina uhakika uswahilini maisha yataendelea, itakua likizo kwetu ya kazini.
Ninyi Mataga mnatakiwa Lockdown ya Magereza sio ya uraiani
 
Ndiyo sababu hao walioko jikoni kutokana na hali halisi wanayoiona huko jikoni wameamua kutoa tahadhari ili tuwe makini zaidi katika kupambana na hili gonjwa.
Mkuu huu ugonjwa upo toka mwaka jana na tumeshuhudia athari nyingi tu kutokana na hatari za huu ugonjwa kutoka kwa wenzetu ila sisi muda wote huu bado tu tunaambiana kuwa waliyoko jikoni ndio wanajua uhalisia wa corona, sasa hii ina maana gani na ni uhalisia upi wanaokutana nao huko jikoni ili nasi tujue?
 
Na ni bora aliwafokea hao maaskofu uchwara.

Hakuna dini inayofundisha kutapeli watu kwa magonjwa ya kuigiza.

Nyinyi madalali na vibaraka wa wazungu kiama chenu hakipo mbali.

Hatuwezi kuruhusu mliangamize taifa kwa machanjo yenye sumu.
Ni ajabu jinsi mtu anaweza kutumia mitambo ya kisasa na kuwa na akili zama za mawe. Huoni Covid mtaani? Sawa. Umeona malaria mtaani? Hapana? Asante, kumbe ni utapeli pia?
Usukari unasemekana unaua watu, lakini hujaona mtaan? Kumbe utapeli bila shaka.
Pia "elimu" hiyo ambayo wanafundisha kuhusu bakteria na virusi. Utapeli tena, maana sijawahi kuona bakteria mtaani.
Asante kaka kwa kutufundisha mantiki!!!
 
Hili la mama kwenda hospital bila ya interijensia yake kumpa full coverage ya eneo husika naona ni mazingaombwe tu.

Hivi ni kweli mama alikuwa hana taarifa za kina juu ya hospital hiyo kabla ya kwenda?

Eti nae anafika ndio anashtukizwa wagonjwa wa corona wapo. Ngoja nichekeko hahahaha
Hilo jambo hata mimi linanishangaza kwa kweli hasa ukizingatia anaonekana kuwa ameamua kupambana na corona.
 
Ni ajabu jinsi mtu anaweza kutumia mitambo ya kisasa na kuwa na akili zama za mawe. Huoni Covid mtaani? Sawa. Umeona malaria mtaani? Hapana? Asante, kumbe ni utapeli pia?
Usukari unasemekana unaua watu, lakini hujaona mtaan? Kumbe utapeli bila shaka.
Pia "elimu" hiyo ambayo wanafundisha kuhusu bakteria na virusi. Utapeli tena, maana sijawahi kuona bakteria mtaani.
Asante kaka kwa kutufundisha mantiki!!!
Malaria au kisukari ni tofauti na corona kama zingekuwa sawa basi hata tusingekuwa tunaizungumzia corona dunia nzima, corona inaambukiza tena kwa kasi na na hakuna dawa tofauti na malaria yenye dawa au hicho kisukari ambacho watu wanaishi nacho miaka.
 
Sawa mama SSH. Siyo kama yule alikuwa anawafokea mpk viongozi wa dini waliovaa barakoa. Alikuwa akiwananga kwamba hawana Imani kwa Mungu wanayemtumikia. Yule yule mtu yule!!!

Kongole mama.
JPM was right. Ni ninyi wenye akili finyu hamkuwa mnamwelewa yule shujaa. Alikuwa mtu aliyejaa Iman kwa Mungu muumba ambaye hashindwi chochote. Corona ni nini mbele zake?.
 
Jiwe mlimjaza sifa za kijinga kama hizi akaacha kuchukuwa tahadhari korona ikampeleka. Kafa kijinga kwa sabb alikuwa mjinga.
 
Back
Top Bottom