Rais Samia toa kauli zenye nguvu na zilizo bayana

Rais Samia toa kauli zenye nguvu na zilizo bayana

Darmian

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2017
Posts
17,289
Reaction score
46,624
Ni vyema Rais Samia wakati wa kutoa maelekezo yake awe anakuwa wazi nini hasa anataka na atoe kauli zenye nguvu ili ujumbe ufike kwa nguvu pia kwa wahusika wote wa pande mbili.

Leo wakati anatoa hotuba yake mara baada ya kuwaapisha Mawaziri na Mwanasheria mkuu wa Serikali alitoa neno kuhusu hili saga la Wamachinga linaloendelea.

Ameonesha hafurahishwi na biashara hiyo inavyofanyika kiholela na inavyovuruga biashara zinazolipa kodi. Lakini aka sugar-coat maneno yake na sijajua ni intentionally au accidentally..Mhe.Rais amesema wapangwe na nguvu isitumike,watolewe kwa amani.

Kitu ambacho hakiwezekani kirahisi hivyo kwa hawa watu na pia kauli hiyo inawapa watekelezaji wakati mgumu na pia kauli hii haiwaandani Wamachinga kutoka sehemu hizo kwa haraka kwa kuhofia matumizi ya nguvu.

Mimi naona ilibidi aseme yafuatayo;

✓ Biashara holela ni marufuku nchini. Watu watafanya biashara kwenye maeneo rasmi tu.

✓ Walioko maeneo yasiyo rasmi kama vile kwenye road reserves,mbele ya fremu za biashara za watu wengine hawaruhusiwi kuendelea na biashara maeneo hayo.

✓ Maafisa wa mipango Miji na Majiji wataelekeza ni maeneo gani rasmi ya kufanya biashara na atakaye kaidi "NGUVU" zaidi itatumika..deadline iwekwe watu wajiandae kuhama.

======

Kauli yake ya leo bado itawapa watekelezaji wakati mgumu..Wamachinga hawa hawataondoka maeneo hayo bila nguvu kubwa kutumika kwa watakaokaidi.
 
Unadhani yeye na chama chake hawapendi kura za machinga? Lazima waache kauli zinaelea hewani ili kesho likibuma wapate upenyo wa kutokea.
If so, basi hii nchi tutakuwa hamna tunachokifanya, na sisiemu baada ya miaka 60 na zaidi wanaendelea kufanya nchi kuwa kama ya watu wasiojielewa kabisa kabisa hata kidogo.

Hawa wamachinga kutapakaa kila sehemu na wanaendelea kuachwa ni bomu kubwa sana.
 
Ishu ya machinga ni ngumu kuitatua.
Ni ngumu ndio ila hatuna budi kufanya sasa hivi wakiachwa hivi na population inazidi kuongezeka hii nchi itakuwa kama jalala..

Najua kila mtu inabidi apeleke mkono kinywani lakini sio kwa kuvurugavuruga utaratibu hivi aisee..Barabara zinatengenezwa then zinaanza kuzibwa tena.
 
Nilihisi sikumuelewa peke yangu..hakufunguka inavopaswa. Machinga ni kero na wanapaswa kutolewa tamko la moja kwa moja,...Mwendazake aliwapa jeuri na kiburi matokeo yake wanajiona wanastahjili kufanya shughuli zao kila mahali, si sawa!
hahahah Mkuu pole leo kama Machinga wangetolewa nilikuwa nakuletea zawadi pale Azam .. pole kwa kukosa zawadi.

Kwenye hili la machinga wewe unasema hivyo kwakuwa huna la kupoteza kabisa, huna ndugu machinga wala hawakugusi wala kukunufaisha kwa lolote.

Kwa Samia yeye swala la machinga linamgusa sana na litamgusa kwa kila njia ambayo itatumika maana itakuwa na matokeo moja kwa moja kwake kuliko yeyote yule.

Rais Samia ujamuelewa kwakuwa wewe unataka aseme moja kwa moja kuwa hataki kuwaona kwenye hayo maeneo kitu ambacho hakiwezekani kabisa.

Rais Samia anajaribu kutaka kuonekana mwema na kila mtu ndio maana umeshindwa kumuelewa lakini kwa kauli yake iko wazi kuwa hawataki wamachinga uko mtaani na ameeleza wazi lakini anajificha ficha kwakuwa anaogopa kuonekana mbaya.

Rais anatakiwa kuwa na msimamo wa wazi kwenye kila jambo sio kukaa katikati kama anavyofanya Rais Samia.
 
Kwa kauli hizi na hayo maagizo yakishindwa kutekelezeka watu wakimwona Mama yetu kama ni "dhaifu" watakuwa wanakosea au watakuwa sawa?
 
Ni ngumu ndio ila hatuna budi kufanya sasa hivi wakiachwa hivi na population inazidi kuongezeka hii nchi itakuwa kama jalala..

Najua kila mtu inabidi apeleke mkono kinywani lakini sio kwa kuvurugavuruga utaratibu hivi aisee..Barabara zinatengenezwa then zinaanza kuzibwa tena.
Hawa hawa wamachinga kuna siku watakuja kuwageuka hawa viongozi na watakimbia maofisi yao yote. Mpaka Ikulu itakimbiwa.
 
Mbona kaweka wazi. Wapangwe vizuri. Maana yake mbele ya frame za biashara nyingine wataondolewa, kwenye road reserves wataondolewa vibanda ambavyo vimejengwa bila vibali vitaondoka, watafutiwe sehemu mwafaka za kufanyia biashara zao. Kipi ambacho hakipo wazi hapo? Nyie mlitaka waswagwe tu kama mtu anaye swaga mifugo yake? Mbona hata mifugo ikiswagwa inakuwa na ulekeo ima inaenda kuchungwa, kupelekwa kwenye kunyweshwa maji, josho, mnadani, machinjioni au kurudishwa zizini. Yuko mwanadamu ambaye thamani yake ni chini ya mifugo?
 
Waboreshe kilimo kwa kukiongezea thamani. Hakutakuwa na machinga tena mjini. Mimi nasimama na machinga, maana ni dada, kaka,baba, na mama zetu. Wanatafuta mkate wao wa kila siku ili kukidhi mahitaji muhimu kwa familia zao. Kwa nature ya biashara zao unawatoa kuwapeleka wapi?
Serikali imeshindwa kuleta maendeleo kwa wananchi wake, na indicator moja wapo ni hilo la watu kukimbilia mijini kutafuta ugali.
Hata zile milioni hamsini walizowahi kuahidi, hakujawahi kutokea utekelezaji wake. Huenda zingesaidia kuboresha maisha ya raia huko vijijini na kupunguza wimbi la raia kukimbilia mijini.
Ukitaka kujua serikali imeshindwa, hata elimu zinazotolewa hazijasaidia watu kijikwamua kimaisha. Wasomi wengi leo ni madereva bodaboda na machinga. Leteni uwekezaji wa viwanda na makampuni kupunguza wimbi la kazi zisizo na kichwa.
Mwisho, hakuna kiongozi wa CCM anayesema ni kwa namna gani watapunguza wimbi la umaskini kwa wananchi wake. Zaidi, serikali iko kuwafanya wazidi kuwa maskini na matozo juu.
Njia iloyobaki ni CCM kupisha wengine, tujaribu vyama vipya na sera mpya.
Natoa rai, machinga komaeni kutetea ugali wenu. Otherwise, waje na way forward ambayo haitoathiri vipato vyenu.
 
Back
Top Bottom