Waboreshe kilimo kwa kukiongezea thamani. Hakutakuwa na machinga tena mjini. Mimi nasimama na machinga, maana ni dada, kaka,baba, na mama zetu. Wanatafuta mkate wao wa kila siku ili kukidhi mahitaji muhimu kwa familia zao. Kwa nature ya biashara zao unawatoa kuwapeleka wapi?
Serikali imeshindwa kuleta maendeleo kwa wananchi wake, na indicator moja wapo ni hilo la watu kukimbilia mijini kutafuta ugali.
Hata zile milioni hamsini walizowahi kuahidi, hakujawahi kutokea utekelezaji wake. Huenda zingesaidia kuboresha maisha ya raia huko vijijini na kupunguza wimbi la raia kukimbilia mijini.
Ukitaka kujua serikali imeshindwa, hata elimu zinazotolewa hazijasaidia watu kijikwamua kimaisha. Wasomi wengi leo ni madereva bodaboda na machinga. Leteni uwekezaji wa viwanda na makampuni kupunguza wimbi la kazi zisizo na kichwa.
Mwisho, hakuna kiongozi wa CCM anayesema ni kwa namna gani watapunguza wimbi la umaskini kwa wananchi wake. Zaidi, serikali iko kuwafanya wazidi kuwa maskini na matozo juu.
Njia iloyobaki ni CCM kupisha wengine, tujaribu vyama vipya na sera mpya.
Natoa rai, machinga komaeni kutetea ugali wenu. Otherwise, waje na way forward ambayo haitoathiri vipato vyenu.