Rais Samia toa kauli zenye nguvu na zilizo bayana

Suala la msingi siyo kukosekana kauli thabiti isiyo na tafsiri zinazokinzana. Lazima tuelewe chimbuko la Umachinga. Hawakuota kama uyoga. Umachinga ni kielelezo cha 'bomu' linalokabili taifa letu - yaani ukosefu wa ajira kwa vijana. Bila kupatikana ufumbuzi wa tatizo hili mengine yote ni ngonjela tu; umachinga utaendelea kutamalaki. Na kweli "ukiwagusa tu utanuka".
 
Point
 
Ni tatizo la kutaka pande zote za shilingi; halafu nimesoma akisema kuwa yeye hafokei watu, ila anatumia kalamu yake. nadhani huo siyo uongozi kwani kama hutoi maagizo thabiti bali unategemea mtu uliyemtuma alete unachotaka bila kumweleza ni nini unataka ama sivyo utamfuta kazi bila hata kumweleza kwa nini umemfuta, hilo ni tatizo.
 
Njia iloyobaki ni CCM kupisha wengine, tujaribu vyama vipya na sera mpya.

hapo ndipo tatizo lilipo; Chama gani kitakachopishwa na CCM iwapo vyama vyenwe ndiyo hivi. Hata kama CCM ingeendelea kuwa Madarakani, iwapo vyama vya upinzani vingekuwa na nguvu, haingefanya hayo yanayolalamikiwa. Zamani sana ilikuwa mtu akionekana na nguo za kijani za CCM anazomewa, leo hii hali siyo hivyo.
 
Mkuu, huna rais wa namna hiyo hapa.

Ni lazima awe 'vague' ili asionekane yeye ndiye mbaya kwa hao walengwa.

Magufuli pamoja na ubabe wake hakuthubutu hata kuwa 'vague', yeye moja kwa moja alitaka sifa zote kutoka kwa hao wafanya biashara.

Huyu mama anataka yeye asilaumiwe. Pakitokea watekelezaji wakafanya lisilowapendeza hao watu, mama mara moja anawaruka. Atasema yeye hakuagiza iwe hivyo. Na kwa upande wa pili, watekelezaji wasipofanya lolote la kuwaondoa hao watu, walalamikiwa watakuwa hao hao watendaji, na mtoa maagizo atawaruka kwa kusema walishindwa kutekeleza maagizo yake.

Viongozi wote dhaifu sifa yao kuu ni hiyo ya kuwa 'vague'; kuepuka lawama toka pande zote.

Hapa sioni chochote kikifanyika kubadilisha hali iliyopo sasa.
 
Wiki iliyopita niliweka Post nikimtaka Mkuu wa Mkoa asikwepe jukumu la kuwaondoa wamachinga, nilisema wazi hakuna mwenye uwezo wa kuwaondoa isipokuwa Rais peke yake, na nilikazia Mkuu wa Mkoa hawezi hasilani. Rais aliwajengea kiburi na wakajengeka na nikasema Makamu wa Rais na Waziri Mkuu hawathubutu kuongelea kuhusu wamachinga kwani liko juu ya uwezo wao, ni wazi Rais kuwaogopa wamachinga kunatia shaka.
Nilimalizia kwa kusema tarehe 13/09/2021 itapita na wamachinga watakuwapo na wataendelea kuwapo.
 
Pia awe muwazi kuhusu katiba mpya na asisingizie kwamba anashughulikia uchumi kwanza.
 
Pia aache kauli za kinyonge mara utasikia "waliniona dhaifu"
Anashangaza sana ujue, sijui watu wa namna hii wanawaokotaga wapi, kutwa anatafuta huruma na jinsia yake. Hii nchi kuja kuendelea bado sana.
 
Unadhani yeye na chama chake hawapendi kura za machinga? Lazima waache kauli zinaelea hewani ili kesho likibuma wapate upenyo wa kutokea.
Huo ndio ukweri 100% ndugu zangu
 
Panya akikuuma huwa anakupuliza ili usisikie maumivu ukiamka nyama ya kisigino cha mguu haipo.

Machinga wajiandae kisaikolojia mama wa kambo si mama.
 
Kwa hili ni sahihi ila kuwatoa pia kuendane pia na kuwapeleka sehemu ambazo zina nafuu na wao wapate chochote..

Hili tatizo limekuwa sugu hatari yaani kuendelea kumung'unya maneno hakutufikishi..

Labda pia tuje na wazo la biashara za ucku Ili wao wafanye biashara ucku asubuh wapishe wengine..

Mwisho watumie njia ya kuwatoza kodi na leseni mambo ya bure hakuna ,bora walipe leseni hata ya 100,000 kwa mwaka au miaka 2 .
 
Huu upuuzi ulidhibitiwa vizuri kipindi cha JK hadi wakawa wanajengewa masoko ila yule mwehu wa huko mapolini alivyokuja akaulea mpaka inaonekana as if ni utaratibu rasmi kwa maelezo eti ni wapiga kura wake..
 
Dawa ya nyie machinga bila kuwawekea kodi au leseni marufuku tena iwe sawa na wenye maduka tuu huwezi sepa
 
Dawa ya nyie machinga bila kuwawekea kodi au leseni marufuku tena iwe sawa na wenye maduka tuu huwezi sepa
Njooni na utatuzi wa kudumu ikiwa mnaona machinga hawachangii pato la taifa. Sio hizo ngonjera za majukwaani. Ukitaka kuona nguvu ya machinga, watimueni. Mimi nasubiri kuona hizo siku saba mlizotoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…