Rais Samia toa kauli zenye nguvu na zilizo bayana

Mnataka afoke foke kama yule kichaa aliyekuwa mtaani kwenu.
Sio afoke bali atoe maagizo yanayoeleweka. Kama sisi huku bado hatujamuelewa hao watendaji watatekeleza nini? Anasema "wamachinga wapangwe vyema" jiulize kuwapanga vyema ndio vipi wakati wanamaeneo rasmi tayari, ni ama atoe amri ya kuwaondoa au awaache sio kutoa maagizo yasiyoeleweka.
 
Kwa kauli hizi na hayo maagizo yakishindwa kutekelezeka watu wakimwona Mama yetu kama ni "dhaifu" watakuwa wanakosea au watakuwa sawa?
Mkuu Wamachinga lazima waondoke katikati ya miji yote nchini. Ni suala la muda tu.
 
Jamaa anahisi mbinu ni kusubiria kura za wamachingaπŸ˜…!!! CCM ina mbinu nyingi mbadala ndio maana still iko madarakani
Na ndio maana ukianza habari za katiba wa warioba ni sawa na kuwashika makalio watakavyokushambulia!!
 
Maeneo rasmi kwenye barabara za gari na njia za waenda kwa miguu? Kama hamjamuelewa endeleeni na shughuli zenu ipo siku mtamuelewa.
 
Maeneo rasmi kwenye barabara za gari na njia za waenda kwa miguu? Kama hamjamuelewa endeleeni na shughuli zenu ipo siku mtamuelewa.
Hujanielewa, point yangu ni kwamba tayari wanamaeneo rasmi kwamba wakitolewa humo barabarani ndio wataenda huko sasa hii kauli ya kuwapanga vyema ina maana gani? Je ina maana kwamba wafunge mitaa kama alivyosema mkuu wa mkoa, wakae barabarani lakini isiwe karibu maduka au wawaelekeze barabara za kufanya biashara. Yeye anatakiwa aseme wamachinga waondolewe au wabaki lakini sio stori za kuwapanga vyema.
 
This is what we are talking about..

Atoe kauli iliyonyooka ili hata hao machinga wajiandae kisaikolojia seriously coz wataona hawana mtu wa kuwatetea kwenye hili kama msimamo wa Rais ni dhabiti kwamba lazima waondoke kwenye sehemu zote zisizokuwa rasmi.
 
Tangu lini ccm wanategemea kura zilizopigwa na wananchi?!!tena wamachinga?!!unatania wewe
Hao wamachinga hata kupiga kura tu huwa hawaendi achilia mbali kuwa kura za Watanzania sio greenlight ya CCM kuingia Ikulu.
 
True..vyama vya upinzani inabidi wajipange watengeneze watu aisee..CDM ya kina Slaa sio hii ya sasa,hii ya sasa imeparanganyika vibaya mno hata tukisema waingie ikulu itakuwa ni utani aisee.
 
Huu upuuzi ulidhibitiwa vizuri kipindi cha JK hadi wakawa wanajengewa masoko ila yule mwehu wa huko mapolini alivyokuja akaulea mpaka inaonekana as if ni utaratibu rasmi kwa maelezo eti ni wapiga kura wake..
Kipindi cha Jk miji ilikuwa safi sana..

Jiwe kuruhusu huu uholela inaonyesha tu ni kiasi gani alikuwa hafai kuwa kiongozi mkuu wa hii nchi..anyway,aendelee kupumzika vyema.
 
Sasa si uwaeleweshe na wengine...
Si tulielewa hivyo.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Miji inanuka kupitia wamachinga. Mikojo inawekwa kwenye chupa za maji, vinyesi kwenye mifuko walio ondoa bidhaa.
 
'vyama vyenyewe ndio hivi... ' , ni kauli potofu. CCM hakuanza kama ilivyo. Vyama vya upinzani vinateswa na serikali ya CCM visikuwe, lakini unaona, vyama vyenyewe ndio hivyo. Viongozi wa upinzani nyumba zao ni mahabusu, sebule zao ni mahakamani, lini watajenga vyama vyao? Viongozi wa CCM wanafanya mikutano na wananchi kila siku, wapinzani hata mikutano ya ndani hawaruhusiwi, wewe unaona vyama vyenyewe ndio hivyo. Ujinga wa watu wa aina yako ndio nguvu ya CCM kuendelea kudumaza maendeleo ya nchi hii.
 
Pia awe muwazi kuhusu katiba mpya na asisingizie kwamba anashughulikia uchumi kwanza.
Kujenga uchumi ni swala endelevu, atafanya sehemu yake na ataondoka. Katiba inahitajika, japo ni mwiba wa samaki kwa CCM.
 
Kwa kweli ni muhimu sana serikali iwe makini na biashara za machinga maani wakiendelea kuwachekea miminiko la vijana kutoka vijijini kwenda mijini litakua tishio.
 
Mama anangata na kupuliza kwa kauli hiyo legalege nani atakayekubali kuondoka kwa amani
 
www unafikiri wataondoka kirahisi hivyo
 
www unafikiri wataondoka kirahisi hivyo

Hakuna njia ya rahisi ya kumuongoza mwanadamu kama utafanikiwa kumuonesha unathamini utu wake, unamuheshimu, kumjali na kumpenda. Zoezi la kuwahamisha wa machinga liwe la ushirikishwaji. Na hapo kwenye kushirikishana na ijulikane kwamba yako mambo serikali itabidi ikompromise.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…