Rais Samia toa kauli zenye nguvu na zilizo bayana

Mbuyu pia huota kama mchicha ila ukishajikita vema kuuondoa lazima kijasho kikutiririke.Hawa wachuuzi walikuwa holela pale mwanzo na walidharaulika(hawakukubalika kama ilivyokuwa kwa Boda Boda) sana na watawala.
Mabadiliko makubwa kwenye hizo Tasnia baada ya mdororo mkubwa wa ajira kwa wananchi,makundi haya yalipoanza kuwaunga mkono wapinzani ndipo CCM kama kawaida yao wakakurupuka na kujipendekeza kwa makundi haya ya jamii.Wakajaribu propaganda za kuwakomboa na kurasimisha kazi hizo bila utafiti wowote Bali mihemko ya kisiasa.Hapo kila kitu kikavurugika,wakaja na viatambulisho Fake na kuwaibia na sasa hawafahamu watawaondoaje/kuwawekea mazingira wezeshi waendelee na shughuli zao!
Prime areas zimevamiwa na biashara zingine zimeathiriwa sana na uholela wa biashara zinazotembezwa.Swali linalowajia watawala ni watawapeleka wapi mamilioni ya Watanzania waliopo kwenye hizo tasnia,mazingira ni wezeshi kiasi gani,utayari wa wahusika kwenda pembezoni na uhakika wa hizo kura.Hali ya CCM na serikali yake ni tete!
 
Ukiwa nyundenyonde, wewe ni nyonde nyonde tuuu
 
Pia awe muwazi kuhusu katiba mpya na asisingizie kwamba anashughulikia uchumi kwanza.
Huwezi kupata uwazi wowote kutoka kwa huyu, itabidi tu watu wamzoee hivyohivyo.

Kwanza ni tabia za kimalezi, tokea utotoni kafundishwa na kuona watu wanaomzunguka wakifanya hivyo, kutokuwa wazi kwa jambo lolote.

Pili, nafasi anayoishikilia sasa hivi imemzidi kimo, anadhani akifanya jambo ambalo halitawapendeza wengi atalaumiwa na kupoteza sifa za kuwa na nafasi hiyo.
 
Rais anaogopa sana lawama..na anajitetea sana kwa maamuzi yake.
 
Rais anaogopa sana lawama..na anajitetea sana kwa maamuzi yake.
 
Kwa hili yuko sahihi
Lazima diplomasia ianze nguvu baadae

kwa sababu alielilea tatizo ni mtu aliekuwa kwenye nafasi kama yake just months ago....

ukikurupuka unaweza usibaki madarakani...ila polepole tutafika...japo natuma pole za dhati kwa machinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…