Rais Samia: Tuache migongano, kusengenyana, uvivu na uzembe ili tufanye kazi za watu

Huku ni kufuja pesa za walipa kodi tu .mpaka mtu anateuliwa kuwa waziri hajui majukmu yake tu mpaka tukamfundishe tena
 
Ni kweli

Maana awamu ya 5 kila kitu walisingizia ni amri kutoka Juu kumbe urongo mtupu

Mfano uwepo wa akina Halima Mdee walisingizia ni amri kutoka kwa Shujaa, lakini mbona bado wanadunda bungeni hadi Kesho!!
Wewe unapajua juu ni wapi?
Juu ni Ikulu inayokaliwa na mwenyekiti wa CCM taifa.
Wewe unataka Halima Mdee na genge lake la Covid 19 wafukuzwe bungeni ili CCM iaibike.
 
Well said, kuna watu wa ovyo sana utasikia amri kutoka juu, ukimuuliza juu kwa nani nimuone hasemi, uoga na kutokujiamini
 
Tutegemee makosa mengi ya wateule wa Rais
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo amefunga Mkutano wa Faragha wa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu Jijini Arusha ambapo amewataka viongozi baada ya kurejea kwenye majukumu yao wakaache migongano, kusengenyana, kuhujumiana, uvivu na uzembe ili wakaaminiane na kushirikiana kufanya kazi za Watu (Wananchi)

Rais Samia amesisitiza kuwa WANANCHI NDIO WENYE NCHI NA HAWAFAI KUDHARAULIWA lakini pia amewataka viongozi kutodharauliana wao kwa wao.
 
Tatizo ni mifumo mibovu, kikifanyika nzuri ni cha Rais, kibovu cha watendaji
 
mwigulu alitudharau eti tuende Burundi
 
Aache kuwaruhusu mawaziri na machawa wake kumkashifu Raia aliyejipumzikia.
 
Dharau ipi kusengenyana ni kawaida.. Aanze na chama chake viongozi aliowateua… Hawa ndio wanawadharau sana wananchi kwa ubadhirifu wa mali na kodi za wananchi. Wamejawa viburi hawa ndio wamewafanya wananchi kuwa maskini kupindukia… Hawajali kwa ufupi… Hawa ndio wanadharau sio wananchi
Kusengenya si jambola kulalamikiwa ni jambo la kawaida katika jamii…
 
Mama yupo sahihi ,Viongozi hawana budi kufanya kazi kwa kufuata Katiba,sheria,taratibu na miongozo ya kazi,lakini moja ya nyenzo MUHIMU kabisa ni kupata KATIBA ILIYO BORA na ambayo upatikanaji wake utakuwa shirikishi

KATIBA MPYA BORA itazaa sheria nzuri,zitakazoleta KANUNI bora kwa wateule wa serikali..

Kanuni hizi zitaelezea kwa ufahasama kazi na mipaka ya kila mteule,anawajibika kwa nani,lakini vile vile itakuwa rahisi kwa mamlaka yake ya uteuzi ,kumpima

Rai kwa Mh Rais,harakisha mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya iliyobora kwa kuwa itakurahisishia utendaji wako wa kazi
 
Kutwaaaa ni msifanye mtajua wenyewe si uwafute kazi ukitiuambia sisi hatuwajui hao amri kutoka juu ni akina nani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…