Rais Samia: TUCTA hawakuja na madai mapya. Kadri uchumi wetu unavyoimarika, tutaendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi wetu

Rais Samia: TUCTA hawakuja na madai mapya. Kadri uchumi wetu unavyoimarika, tutaendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi wetu

Dalili zilionekana tangu awali kwamba kusingekuwa na nyongeza kwenye maslahi ya watumishi kwa mwaka huu, kutokana na;
1. Athari za Vita ya Israel na Irani
2. Uchaguzi wa mwaka Jana 2025

Kwasisi wasoma alama za nyakati, kutakuwa na maboresho ya maslahi mwaka 2029

Hapa katikati ni kuishi kwa matumaini tu
Hili ndilo lililokuwa kichwani mwangu exactly, na lipo obvious sana tu.

Nashangaa sana namna watu wasivyoweza kusoma upepo kabisa! Kuna wadau wamesafiri huku umbali mrefu eti wanaenda kwenye maadhimisho kimkoa wamepigilia mitumba yao ya tughe, cwt na talgwu wana matumaini ya kuambulia chochote mwaka huu!
 
Hakika Mkuu

Ili kutokuwa disappointedly na hawa wanasiasa wetu, vyema watumishi kuanza kuwa na vibiashara nje utumishi wao

Hata biashara ya kuingizia 15,000 kwa siku

Mathalani ukiwa na saluni uchwara za Kiume mbili, huwezi kukosa shilingi 7,000 kwa Kila moja

Huo ni uwekezaji ambao hauzidi shilingi milioni 2
 
Ongezeko la Mshahara private sector= Major Retrenchments....kuna watu wameshangilia.
 
1777641276939.jpeg
 
Rais Samia Suluhu Hassan akishiriki Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani inayoadhimishwa Kitaifa Mkoani Njombe, leo tarehe 1 Mei, 2026 amesema kuwa mwaka huu hakutakuwa na maboresho ya maslahi ya wafanyakazi kwasababu mbalimbali ambazo ametaka kuwa TUCTA hawakuja na madai mapya bali walimpa pole kwani nchi imetoka kwenye uchaguzi na gharama kubwa zimetumika kufanikisha uchaguzi huo.

Sababu nyingine ni mabadiliko ya kisiasa na chumi ambazo pia zimeathiri uchumi wa nchi

Ameongeza kuwa nchi imepata uharibifu mkubwa wa mali uliotokana na vurugu za uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025, lakini pia miundombinu kutokana na mvua kubwa nchini hivyo hela inayopatikana inapelekwa katika kurekebisha miundombinu

Sababu nyingine ni kulipa kwanza madeni ya wafanyakazi, wakandarasi ili tunapoanza utekelezaji wa dira mpya tuanze tukiwa na mwelekeo mzuri unaoeleweka.

Pia soma: Rais Mwinyi aongeza kima cha chini cha mshahara kutoka 300,000 kwenda 500,000
Sawa tu, mpaka Watanganyika vichwa vyao vikae vizuri.

Wakati mwingine, ili awe tayari kuchukua hatua ya kujikomboa, mtu lazima apitishwe kwenye tanuru la moto!
 
Back
Top Bottom