Rais Samia, tufuate utaratibu huu; migogoro yote itaisha nchini

Rais Samia, tufuate utaratibu huu; migogoro yote itaisha nchini

CCM Music

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2018
Posts
1,036
Reaction score
1,784
Naam, jamaa ni yule yule sijui ni wale wale I don't know.

Namna ya kutatua migogoro ya Ardhi nchini.

Jisomee mwenyewe.

Halafu, wapinzani njooni kosoeni tuone hoja zenu na CCM tuchukue

==========

MIGOGORO YA ARDHI – TANZANIA

(Kumradhi Mama, naomba niandike kwa lugha za vijana wa mitandaoni)

Mama Shikamoo!

Hatuhitaji mambo mengi Mama kutatua changamoto mbali mbali hapa Tanzania. Tunahitaji kuwa na utashi tu, Mama.

TUFUATE UTARATIBU HUU, MIGOGORO YOTE ITAISHA NCHINI.

Kila Mjumbe kwenye sehemu husika ahakikishe kuwa ardhi ya pahala anapohusika anafahamu kwa uhakika mmiliki wake wa kweli. Mjumbe anakuwa na orodha ya wamiliki wa ardhi kwenye eneo lake.

Kwa maeneo yenye migogoro, Mjumbe anapaswa kuwa na orodha ya maeneo ya migogoro.

Wenye migogoro kwenye eneo husika pia hubainishwa kwenye orodha yao.

Kila mjumbe ahakikishe kuwa orodha yake aliyo nayo ya wamiliki wa ardhi inapelekwa serikali za mitaa husika. Hii ni pamoja na orodha ya maeneo yenye migogoro na wenye migogoro kwa ajili ya database.

Serikali ya mtaa hupaswa kubandika kwenye ubao maalum (pamoja na kutunza kumbukumbu zake za kiofisi) orodha ya wamiliki ardhi kwenye eneo husika pamoja na maeneo yenye migogoro pamoja na wenye hiyo migogoro.

Serikali ya mtaa huwasilisha orodha zote kwenye vitengo vya ardhi kwenye kata, na pia kwenye wilaya/halmashauri/manispaa. Kata na halmashauri nao huweka kumbukumbu ya orodha hio. Kata wanapaswa kubandika kumbukumbu hizo ubaoni.

Orodha waliyopewa wilayani / halmashauri kutoka kata ama serikali ya mtaa nayo hupelekwa wizarani kwa kumbukumbu zaidi.

Kila kata kuwe na ofisi moja ya mawakili wanaoshughulika na uuzaji wa ardhi. Tunasema ofisi moja ili kuondoa mikanganyiko kwenye kuuziana na kununua ambako ndipo chimbuko la migogoro. Hii itasaidia kwamba hata ukitaka kwenda kununua ama kuuza ardhi ni rahisi mawakili hao kufahamu kama ardhi hio ilishauzwa ama la, na hivyo kuepuka udanganyifu wa namna yeyote ile.

Ofisi hii ina wajibu wa kuwa na database ya umiliki wa ardhi kwenye kata husika kwa mtiririko wa wajumbe na mitaa pia. Mawakili ni watu tunaowaamini sana.

Ukitaka kununua ardhi unaenda kwa mjumbe na kuangalia kama bado haijauzwa, kisha kuhakiki zaidi kwa mawakili wa kata wanaohusika na ardhi. Ukishajiridhisha sasa upo tayari kununua ardhi husika.

Tafsiri yake ni kwamba, kumbukumbu ya umiliki wa ardhi inaanzia kwa mjumbe, kwenda serikali za mitaa, halafu kata, then wilayani / halmashauri na hatimaye wizarani bila kusahau ofisi za mawakili wa kata.

Mjumbe, serikali za mitaa, kata, ofisi za mawakili, wilayani / halmashauri hadi wizarani wana wajibu wa kuhakikisha kila mwisho wa mwezi (yaani mara 12 kwa mwaka) wana update orodha yao kutokana na mabadiliko yanavyotokea. Hata kama kutakuwa na uzembe kwenye ku update ofisi ya mawakili lazima itajikuta inaji update automatically kutokana na kuhusika moja kwa moja kwenye kuuziana na kununua ardhi. Penye migogoro huendelea kutatuliwa kwa namna wanavyoona inafaa.

# Suluhu is the legacy of Samia. # New Tanzania – Tanzania Mpya ya Samia

Wasalaam,

ONE VOTE COUNTS TANZANIA (IDARA KUU HUDUMA KWA WANANCHI–TANZANIA). Twitter: ovctanzania, Instagram: ovctanzania, Email: ovctanzania@gmail.com SIMU: +255 (0) 785 29 45 45.

Dedication: Rais Mstaafu J. M. Kikwete (nilisikia msibani kwa JPM akiongea kuhusu migogoro ya ardhi)
 

Attachments

Serikali ya CCM najua ni sikivu haiwezi kuacha huu ushauri upotelee gizani
 
Back
Top Bottom