Rais Samia: Tumeshalipia treni 19 za Umeme na mabehewa 89, Seti 10 za treni na mabehewa 80 kwaajili ya mizigo

Rais Samia: Tumeshalipia treni 19 za Umeme na mabehewa 89, Seti 10 za treni na mabehewa 80 kwaajili ya mizigo

IMG-20220204-WA0042.jpg
 
Mama huyu ni jembe kwelikweli, Waliosema miradi itakwama wako wapi?
 
Ndo maana nasema , tz bado hutajapata watu sahii, katika mifumo yetu, unalipia tren za umeme pesa inabaki tu WAKATI mradi wa reli bado, achana na changamoto ya umeme, sijui zitakua zatumia umeme wa kufua zenyewe,

Tunakimbizana lipia kitu ambacho hakianzi kesho fanya kazi wakati ,zipo Sehem kibao kunauhitaji wa kuelekeza pesa, then matokeo yake tozo, kukimbilia kukopa

Tatizo nilionalo ni Kwamba , tunashindwa kutambua kipi kianze ,na kifuatie kipi katika matumizi ya pesa,

Mfano unanunua ndege keshi, kumbe unaweza kuzikopa ukawa unalipa kidogodogo
Wewe unapendekeza kipi kianze???
 
Wewe unapendekeza kipi kianze???
Hatuna sababu ya kulipa kesh katika mradi hauwanzi kesho,japo ni mzuri, mapedekezo yangu pesa ikawekezwe KWANZA katika Mambo ya msingi mfano umeme,maji wakati huo tunao mkataba nao ambao tunaendelea utekeleza taratibu kadiri mradi wa reli unavyoenda,taifa hili bado maskin Sana mkuu
 
mradipic

===
Serikali ya Tanzania imesema imeingia mkataba wa ununuzi wa mabehewa ya abiria 89, vichwa vya treni ya umeme 19, seti za treni za kisasa 10 zenye behewa 80 vikiwa na gharama ya US$381,428,465 karibu TZS 880BL,

Hayo yamebainishwa leo siku ya Jumanne Desemba 28, 2021 na Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan katika hafla ya utiaji saini mkataba wa Ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha tatu kutoka Makutupora hadi Tabora.

Kipande hiki kina urefu wa kilometa 368, kitakachogharimu Dola za Marekani bilioni 1.908 sawa Sh4.41 trilioni kati ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Yapi Merkez kutoka Uturuki.

Amesema pamoja na hayo Serikali inaendelea kukamilisha ununuzi wa mabehewa ya mizigo 1,430 yenye thamani dola za Marekani US$127,206,300 sawa na TZS 292BL,

“Nitumie fursa hii kuagiza wizara na TRC kuhakikisha kuwa inasimamia kwa karibu ili kasi ya ujenzi iendane na kasi ya kusimamia ununuzi wa vifaa hivyo"

"Hii itafanya vifaa viwe vimekamilika sambamba na kukamilika kwa ujenzi wa reli. Vinginevyo miundombinu ya reli itakamilika huku tukisubiri kuwasili kwa vifaa na kuhakikisha ubora unaendana na thamani ya fedha."

“Nasema hivi kwa sababu miezi michache nimekaa katika Serikali hii nimeona kuna mambo yanataka kuanza kufanyika na mimi sitakubali yafanyike"

"Kwamba mradi unasimamiwa na wizara kupitia sekta husika, anatafutwa mkandarasi anapopatikana anakuwa na wasemaji wengi ndani ya nchi, na hasemewi bure watu wanajua watavuna"

"Sasa nasema mimi sijali mkandarasi atasemewa na watu elfu ninachotaka kusema nataka reli iwe ya viwango tulivyokubaliana,” amesisitiza

===
Wonderful Madame Samia
 
Back
Top Bottom