Black Butterfly
Senior Member
- Aug 31, 2022
- 130
- 368
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezungumza na wananchi wa Dumila mkoani Morogoro na kuwaunga kwa kununua nyanya, bamia, tangawizi, mahindi yeboyebo na vitu vingine vilivyokuwa vikiuzwa na wajasiliamali wadogo wadogo pamoja na kuwapatia shilingi milioni 20 kwa ajili ya genge lao.
Aidha Rais Samia amewataka wakazi hao kuchagua viongozi wazuri katika uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa ambao watamsaidia kuwafikishia maendeleo.