Rais Samia: Tunahitaji mfumo wa kisasa unaotenda haki na unaoeleweka kwa walipa kodi

Rais Samia: Tunahitaji mfumo wa kisasa unaotenda haki na unaoeleweka kwa walipa kodi

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 30 ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rais Samia amesema uchumi wa nchi unaendelea kukua kwa kasi huku fursa za biashara zikizidi kufunguka, hivyo ni muhimu mfumo wa kodi uboreshwe na kuendana na mahitaji ya sasa ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato na kuchochea maendeleo ya taifa.

Miongo hii mitatu ni kipindi kilichopita kimetupa uzoefu lakini kimetupa fursa kujitathmini, kujipanga upya na kuimarisha zaidi taasisi yetu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania. Uchumi wetu unakuwa kwa kasi, biashara zinazidi kufunguka na kwa namna hiyo hiyo mfumo wetu wa kodi hauna budi kubadilika kuendana na wakati tulio nao.

Soma Pia: Kuanzia Julai 2025 mpaka Juni 30, 2026, TRA kwa bara na Zanzibar imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 37 na bilioni 957

Tunahitaji mfumo wa kisasa unaotenda haki na unaoeleweka. Nakumbuka kuwa mwezi Julai mwaka juzi 2024 tuliunda tume ya kufanya tathmini ya mfumo wa kodi nchini ambayo imetoa mapendekezo kadhaa ambayo yakitekelezwa tutaunda mfumo unaohamasisha na kurahisisha ulipaji wa kodi na kuwafanya walipa kodi kutambua kwamba kulipa kodi ni wajibu, ni uzalendo na ni kutunza heshima ya taifa letu."

MAWAZO YA UWANDISHI WAKO BADO NI MGANDO - Huwezi kuandika hoja nzito kama hii bila kupangilia hoja zako kwa mantiki ya msingi kama msomi mzuri - Unakuwa kama hujataka kuandika andiko kama msomi huru nadhani ujitafakari mwandishi kwa hilo maana upo very poor kabisa katika andiko lako unakuwa kama sio msomi au mtu umeenda shule kabisa .....
 
He he Mimi mwenyewe nimeshangaa , kutakuwa Kuna sababu ..
 
Back
Top Bottom