Rais Samia tunaomba umtumbue Mkuu wa mkoa wa Tabora hatoshi pale

Rais Samia tunaomba umtumbue Mkuu wa mkoa wa Tabora hatoshi pale

Ijapokuwa sipendi kiburi cha uto na mashabiki wake lakini Rc kaenda mbali sana katika Hilo suala
 
Bwana Paul Chacha ni mkuu wa mkoa ambaye anamchafua mheshimiwa Rais Samia makusudi

Analeta ubabe wake wa Kikurya kwenye mambo ya football

Alitukana Yanga wana kiherehere na wanahonga wachezaji, ambazo hizo ni Tuhuma chafu sana alitaka ajibiwe vipi?
Yaani aje kishabiki halafu kumjibu Yanga waogope cheo chake au v8 ya serikali, hiyo ni never

Viongozi kuwa na upande sio dhambi, mbona wapo na wanaheshika kuwa wapo aidha Simba au Yanga

Waziri Mkuu Casim Majaliwa huyu anajulikana ni Simba na Kwa mamlaka yake angeweza kuwa anawaweka kizuizini viongozi wa Yanga ila yupo vizuri, anapata heshima ya mashabiki wa Simba na Yanga na hajawahi kutoa kauli za kukejeli Yanga, na pia ni mlezi wa Namungo FC

Speaker wa Bunge Tulia Akson ni kiongozi mkuu wa mhimili wa Bunge lakini hakuwahi kuongelea vibaya Yanga japo ni Shabiki wa Simba kindakindaki, Huwa anawaalika Yanga bungeni, Kwa mamlaka yake angezuia Yanga wasifike hata Bungeni

Mh Ali Zungu naibu speaker huyu ni mbunge wa Ilala, zinapotoka Simba na Yanga zipo kwenye Jimbo lake ila hajawahi kutoa kauli ya kifedhuli dhidi ya Yanga na anaheshimika vizuri tu

Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu Huyu ni Yanga lakini hajawahi kutoa kauli ya kipumbavu au maudhi Kwa Simba, kipindi chake Simba alitawala soccer la TANZANIA lakini hakuleta hujuma na kuibeba Yanga

Mwana FA, huyu ni naibu waziri wa michezo na m Wanachama wa Simba pamoja na yote hajawahi kutoa kauli ya kipumbavu dhidi ya Yanga na anaheshimika vyema

Albert Chalamila Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam huyu ni Yanga na timu zote zinatokea mkoa wake haijawahi kutoa kauli ya kipumbavu Kwa Simba, na wanasimba wanamheshimunpamoja na kujua kama yeye ni Yanga

Jerson Musigwa, karibu wa Wizara ya Michezo huyu ni Yanga ila anaheshimika na Simba Kwa kuwa ana busara

Tabora sio timu pekee ambayo Yanga amecheza
Yanga amecheza na Namungo Lindi,
Yanga amecheza na Fountain Gate Manyara
Yanga amecheza dhidi Singida Black Star Singada
Yanga amecheza na Coast union Tanga
Yanga amecheza na Kagere sugar Kagera
Yanga amechezana prison Mbeya
Yanga mecheza na Pamba Mwanza
Yanga amecheza na Mashujaa Kigoma

Mbona huku kote watendaji wa Yanga hawakugombana na wateule wa mheshimiwa Rais

Rais Samia tengua Chacha Tabora naamini una Stock ya watendaji wengine wenye hekima na busara
Kabisa mtu analeta ushamba kwenye mpira kama hawezi mambo ya mpira si akae kimya afanye siasa, atolewe
 
Eti Rais amtengue, kwa kosa gani,?

Mheshimiwa Chacha we shikilia hapo hapo.

Uto-Sasa na hili nendeni CAS tena.
Hili si la CAS. Mahakama zetu hizi hizi, tunampiga madai kwa udhalilishali wa kumuweka ndani msemaji na kuichafua klabu kwa kuisingizia rushwa,au jinai ya kutumia madaraka vibaya.
Tunamuunganisha RPC wake akakaririshwe vifungu vya piijiio
 
We bwege mkuu wa mkoa ni mtu mkubwa, yuko pale kwa niaba ya Rais, mlivyo hamna adabu mtakuja kumtukana ht Rais kisa ushabiki. Tabora ni mkoa wake kiutawala lazima mumheshimu. Katoto km Ally Kamwe ni wa kumtukana RC? Kwanza ht kiumri ni km babake, hii nchi mnataka kuipeleka wapi nyie vitoto vyenye laana? Utafikiri mmezaliwa jalalani. Umeandika matope nyambaf we
Kwaiyo Rais amemteua atukane wananchi wana kiherehere na adhalilishe timu kuwa Kuna rushwa, kama Kuna rushwa aitishe vyombo achunguze

Rais Samia mbona hatukani watu na tunaheshimu vizuri
 
Back
Top Bottom