Rais Samia, tunataka katiba mpya kabla ya uchaguzi wa mwaka 2025

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Mhe. Rais, sisi wananchi kwa ujumla tunakuomba kwa heshima na taadhima iwe jua na iwe mvua tunataka Katiba Mpya kabla ya 2025.

Usemi kuwa wananchi wanataka elimu kwanza kuhusu Katiba Mpya usemi huo hauingii akilini mwetu tunataka Katiba kabla ya uchaguzi 2025 ili nchi iendelee kuwa na amani na CCM iendelee kutawala.

Achana na ushauri ambao kwa namna nyingine hauna tija kuwa kuwe na elimu kwanza. Mhe. Rais tunataka Katiba Mpya kabla ya uchaguzi 2025.
 
Nadhani amekusikia. Hebu subiri kwanza tuone.
 
Unaweza kuwa ulimpigia kura rais SSH lakini huna uwezo wa kumshurutisha nini afanye na nini asifanye, ana miliki vyombo vyote vya dola na hafanyi kazi kwa kumsikiliza kila mtu mtaani anasema nini.
 

Hii inaitwa dua la kuku ..
 
Mama naye ni wale wale
 
Endeleeni kutaka.Kitila amesema wale wanaotegemea huruma ya ccm hawajitambui.
 
Shida ya upinzani wanahitaji katiba mpya wakiamini itawafanya waende Ikulu, ila hawajali kama hio katiba itakuwa inclusive ya kila kitu ? Wao wanataka katiba and specifically wanataka tume ya uchaguzi tu, hawataki vitu vingine
 
Jisemee mwenyewe ikiwezekana na familia yako, wewe hujatumwa na Watanzania.

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…