Ni wizi aisee. Ukifika getini na tiketi ya safari wanakuuliza ulikatia wapi hiyo tiketi, ukisema kwenye booking offices nje ya stendi wanakutaka ulipe Tshs. 300, ili usilipe basi sema umekata ghorofa ya pili zilipo office za mabasi ndani ya magufuli terminal.
Haya sasa, maana ya kiingilio ni kuwa kuna huduma ndani utazipata bila kulipia tena, huduma kama choo, kunawa mikono nk lakini sasa hapo Magufuli bado ukienda chooni unatakiwa kulipa tena kwa huduma ya choo, sasa kiingilio ni cha nini ikiwa huduma bado unazilipia? Wizi
Hongera sana
MUSHEKY kwa uzi huu na kwa kukomaa kutetea haki na msimamo wako kutoporwa hela kizembe. Taifa linajitaji watu kama wewe wa kuhoji uhalali wa mambo na siyo wale wa ndio mzee au bora liende tu.