Rais Samia tupia jicho kituo kikuu cha mabasi cha Magufuli, Mbezi

Mkuu mimi sikuwalipa ila wananchi waliowengi wameshaanzishiwa tozo hii mpya na wanalipa na wengi kwa sababu ya haraka kuwahi usafiri wanaamua kukubali yaishe
Mia tatu ilikuwepo toka ubungo au kuna nyingine imeongezeka mbali na hii tuliokuwa tunailipia.
 
Akili za viongozi wetu ni za hovyo haijawahi kutokea, pale getini ni full wizi unafanyika, ikumbukwe stand zingine zote nchini abiria anaingia ndani kwa ticket yake hata UBT ilikuwa hivyo, hizi ndizo kero tulitarajia RC azishughulikie badala ya kukimbizana na abiria wanaosaidiwa na wasafirishaji, kinachoonekana pale Mbezi ni kukosekana kwa viongozi wenye akili wala siyo elimu, huwa sielewi hivi hakuna policy ya stand zote nchini? Kuna vijitu vijingavijinga vimepewa mamlaka lakini havina uelewa wa mambo gani yafanyike namna gani, hili tatizo Waziri, KM na watendaji wengine wanalifahamu ila kwakuwa aana viini vya tamaa na wizi wamenyamaza kimya
 
Mkuu rejea kusoma nilichoandika..
Nimesema mtu umeshalipia ticket ya basi unayo mkononi..iwaje tena ulipie gate pass
 
Mkuu huyo jamaa mawazo yake yameganda

Hajui kua 300 ya pale ni milioni 300 kwa mwezi
 
Mkuu mimi hawakuniuliza umekatia wapi

Wananiambia eti tiketi yangu sio ya kielectroniki eti ndio sababu

Hili ni genge jipya pa wapigaji tulikemee

Wanafanya hivi kwa kua wanajua tawala zimebadilika so kna mambo wayapenyeze chap

Najua kuna wazee wa kitengo wanapitia uzi huu mpenyezeeni mama hili wananchi tunaibiwa
 
Wanaosema 300 ndogo sio ya kuandikia uzi walitaka aandikie uzi kwa sh ngapi?

Basi hilo jibu lako kuna wengine kwa uwezo wao nao wanaiona hiyo hela kama wewe unavyoiona 300
Ni upeo mdogo tu mkuu, hata mafuta ya petroli na dizeli hupanda kwa kuongezwa hizohizo 100 ila impact zake kwenye uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla ni kubwa mno
 
Sijawahi elewa ni kwa nini watu wanalipishwa ushuru kuingia stand wakati magari tayari yanalipa..

Huu ni wizi harafu mnaita vyanzo vya mapato,stupid..

Kuna wizi mwingine eti Halmashauri zinajenga parking zao harafu wanalazimisha malori
 
Ni kwa vile wameshatuona watz tu wajinga. Wanatuibia kila kona hatulalamiki.

Ukiingia stand kama hotelini, huduma ya Choo ilitakiwa iwe inahesabiwa katika kiingilio chako. Lakini wapi!
Wamezidi tukiendelea kukaa kimya tunaweza kuzikwa tukiwa hai

Kuna watu wana roho mbaya sana kama hii pumzi angeipewa mwanadam aicontrol basi maskini wangefutika
 
Mia tatu ilikuwepo toka ubungo au kuna nyingine imeongezeka mbali na hii tuliokuwa tunailipia.
Ni kweli mia3 ilikuepo toka ubungo ila ni kwa mtu asiyekua na tiketi mkononi ya basi husika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…