Rais Samia: Tutaanza kutoa Tsh 10,000/= kwa siku kwenye pesa za kujikimu (Boom) kwa wanachuo

Rais Samia: Tutaanza kutoa Tsh 10,000/= kwa siku kwenye pesa za kujikimu (Boom) kwa wanachuo

Wasomi wa nchi hii hasa hii miaka ya karibuni ni wa ajabu sana sujui hata kama wana reason, ni hatari sana kuwa na wasomi wa aina hii ambao kureson ni tatizo.

Walipaswa kumbana Mama kuhusu gharama za vyakula, hio 10, 000/ ni sawa na tone Baharini, hakuna kitu hapo kama coast of living zitakuwa juu,

Nchi zingine Serikali huogopa vitu vikuu vitatu;
1. Maandamano ya kulalamikie bei ya vyakula, haya yanaogopwa kama ukoma.

2. Maandamano ya wanafunzi, haya pia ni aina ya maandamano yanayo ogopwa sana.

3.Maandamano ya Wakulima kudai vitu kama pembejea na sera zingine za kilimo.

Hivyo vitu vitatu huwa unaweza shangaa Serikali imepinduliwa.

Ila sasa kwa Bongo hilo halipo, make kama wasomi hata kureson ni shida haw come waingie mitaani.
 
Kuna wasio pata hata shilingi moja na kweli wazazi wao wana uwezo kwelikweli.

Lakini pia kuna wanafunzi wenye wazazi wasio na uwezo na hawapati hata thumni.

Huo utaratibu wa mikopo uchunguzwe. Hautendi haki.
 
Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kaongeza pesa ya kujikimu(BOOM) kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka 8,500 kwa siku mpaka kufikia 10,000/= kwa siku, Hii ni tofauti kabisaa na ilivyozoeleka miaka ya huko nyuma tangu 1990+ mikopo hii ilipoanza kutolewa,

Ongezeko la pesa hii limekuwa likifanyika baada ya fujo, maandamano na mivutano mikali kati ya serikali za wanafunzi, Bodi ya mikopo & serikali kiujumla, Wanafunzi wengi wamepoteza masomo miaka ya nyuma sababu ya kudai ongezeko la pesa hii bila mafanikio

Mara ya mwisho kushuhudia ongezeko la BOOM ilikuwa mwaka 2015 ambapo serikali ya awamu ya Nne iliongeza kiasi cha Shillingi Elfu moja, yaani kutoka 7,500 na kuwa 8,500 ambayo ndio imekuwepo mpaka hapo jana

Bila maandamano, bila migomo wala mvutano wowote Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kaongeza pesa hii kwa takriban asilimia ishirini (20%), Hili ni jambo kubwa kabisaa la kupongezwa, Mama anaendeleza kuonesha UTU, Mama anaendelea kuonesha namna anavyojali Wanafunzi na watanzania kiujumla, Mama amekuwa msikivu wa vilio vidogo na vikubwa

Mama yetu amekuwa sauti ya wasio na sauti, Mama yetu amekuwa mfariji kwa watanzania hakika, In fact she is our comforter in chief, Faraja na Upendo huu alionesha kwa wanafunzi vyuoni ni wa kihistoria. Nchi inakwenda vizuri HAKUNA KILICHOSIMAMA na Kazi inaendelea[emoji1303]

#NJE YA CHAKI
#Malima Chacha
 
Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kaongeza pesa ya kujikimu(BOOM) kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka 8,500 kwa siku mpaka kufikia 10,000/= kwa siku, Hii ni tofauti kabisaa na ilivyozoeleka miaka ya huko nyuma tangu 1990+ mikopo hii ilipoanza kutolewa..
Yaan mama labda damu yake tu haieleweki,anajitahidi saaaàaaaana ila hapendwi Kwa nn hapendwi basi tu hapendwi
 
Huyu Mama, Mungu amzidishie kwa kweli. Nilikuwa na lideni limenielemea na mkataba kazini ulikua umeisha ila baada ya kutuondelea retention fee nikajikuta mambo safi.

Mungu akuzidishie zaidi Mama yetu. Nikimfikiriaga nakosa cha kusema zaidi ya kumuombea kwa Mungu.
 
Maumivu kwa wanufaika ni wakati wa kuanza makato yake sasa! 15% ya makato kwenye basic salary, si mchezo. Ahueni sisi wa boom la 2500 kwa siku, tulimaliza mapema sana.
 
Mwaka huu kalibu nusu ya wanafunzi Mwaka wa kwanza wamepunguziwa ada, unakuta Mwanafunzi kalipiwa laki mbili na board wakat ada ya chuo ni M1.5, pia ndio Mwaka amabao robotatu ya wanafunzi Mwaka wa kwanza hawana industrial training allowance (field). Labda kaamua awafute machozi kivingine.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Mwaka huu kalibu nusu ya wanafunzi Mwaka wa kwanza wamepunguziwa ada, unakuta Mwanafunzi kalipiwa laki mbili na board wakat ada ya chuo ni M1.5, pia ndio Mwaka amabao robotatu ya wanafunzi Mwaka wa kwanza hawana industrial training allowance (field). Labda kaamua awafute machozi kivingine.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Hiyo inaitwa toa pesa Mfuko wa shati weka mfuko wa kaptura
 
Mwanzo ilikuwa sh ngapi? 10, 000/ ni ndogo sana kwa life ya chuo, huwezi ongeza pesa unaacha kudili na mifumuko ya bei hasa ya Chakula, ni ujinga na sijui kama kuna wasomi
Hakuna kitu au kero ambayo haijagiswa na mh Rais Samia na kupatiwa majibu kwa watanzania
 
Kuna wasio pata hata shilingi moja na kweli wazazi wao wana uwezo kwelikweli.

Lakini pia kuna wanafunzi wenye wazazi wasio na uwezo na hawapati hata thumni.

Huo utaratibu wa mikopo uchunguzwe. Hautendi haki.
Kunakuwaga na nafasi ya kukata rufaa kwa mwanafunzi anayeona Anastahili kupewa mkopo lakini amekosa
 
Naona umeweka namba ya simu ili ufuatwe sio na wenye hoja, ila watakaosikia ukijikomba. Acheni ujinga. Huyo Rais unaempaka mafuta kwa mgongo wa chupa hakubaliani na wewe.
Mimi naeleza ukweli tu wa namna vijana na mamillion ya watanzania wanavyomkubali mh Rais kutokana na utendaji kazi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti
 
Dkt. Mama Samia Suluhu Hassan, Mwenyezi Mungu alimteua na kumfanya Rais wa watanzania, amin amin nawaambieni, asiyeamini Mama Samia ni chaguo la Mwenyezi Mungu mwenyewe, pepo hataliona milele..

Mungu wetu mwenye upendo sana na nchi yetu Tanzania, uzidi kumbariki Mama huyo na tunazidi kuona wazi wazi kwa macho yetu upendo wako Mwenyezi Mungu kupitia kwa Mama Samia, amen
 
Back
Top Bottom