GE2025 Rais Samia: Tutaanzisha kituo cha kuenzi tunu za Muungano wetu

GE2025 Rais Samia: Tutaanzisha kituo cha kuenzi tunu za Muungano wetu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewaeleza wakazi wa Mkoa wa Kusini Unguja kuwa endapo watampa ridhaa ya kuongoza nchi, serikali yake itajenga Kituo cha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa ajili ya kuenzi na kulinda tunu za muungano huo.

Dkt. Samia ametoa ahadi hiyo leo Septemba 17, 2025, katika kampeni zake kwa Mkoa huo, kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba.

Ameeleza kuwa miongoni mwa mambo makubwa ambayo chama chake kinajivunia ni kuenzi tunu za muungano wa Tanganyika na Zanzibar, uhuru, Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, amani na umoja. Amesisitiza kuwa CCM ikipewa tena ridhaa ya kuongoza nchi, itaendelea kuyadumisha na kuyaenzi mambo hayo kwa bidii kubwa.

Aidha, amesema kituo cha muungano wa Tanganyika na Zanzibar kitakuwa chenye jukumu la kutunza kumbukumbu za waasisi wa muungano, pamoja na kutoa elimu kwa wageni kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi, ili kukuza uelewa kuhusu historia ya muungano huo na namna unavyoendelezwa.

 
Wacha wee watu wanatunyonya mpaka mpaka kituo cha kuenzi muungano mnataka mtengeneze na shida zote tulizonazo kweli ....Tanzania visiwani mmeula round hiii
 
Back
Top Bottom