Rais Samia: Ufaransa wako tayari kutupa ruzuku na mikopo zaidi

Rais Samia: Ufaransa wako tayari kutupa ruzuku na mikopo zaidi

Kuna muda mtu unatamani kulia, shida ni hata hautaeleweka unalilia nini......

Bantu Lady tumepata chimbo jipya la kukopa
Evelyn ukiwawaza sana Hawa utapata mshtuko wa moyo. Nikuambie tu nchi imefika nafikiri 50% imeuzwa ..njoo pm tutafute Chaka la kupiga pesa billions tutokomee ughaibuni
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ina maendeleo hivyo amewaomba Watanzania kuendelea kuitunza amani nchini na utulivu wa kisiasa na kwamba Watu wasilazimishe vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua ambazo zinaepukika.

Akiongea Jijini Mwanza June 20,2025 wakati akizindua mradi mkubwa wa maji wa Butimba, Rais Samia amesema “Ndugu zangu kama ni maendeleo Tanzania ina maendeleo, kama ni utashi wa kisiasa, utashi wa kisiasa wa kuleta maendeleo ndani ya Tanzania upo na utaendelea kuwepo, niwaombe Ndugu tutunze sifa ya nchi yetu, amani na utulivu, tulete utulivu wa kisiasa, nchi yetu ibakie kuwa na amani ili tusilazimishe vyombo hivi vya ulinzi na usalama kufanya mengine, tutulie, tufanye kazi zetu Tanzania”

“Mmemsikia Balozi hapa wa Ufaransa ameisifu sana Tanzania tulivu na kwasababu ya utulivu wetu, maendeleo yanayoendelea wao wapo tayari kutupa ruzuku na mikopo zaidi ili maendeleo zaidi yafanyike, tukianza kutawanyana hapa hakuna litakalofanyika na hili ndilo wengine wanapenda litokee niwaombe sana Ndugu zangu tuweke sifa ya nchi yetu, Tanzania ni salama twende tukakae salama”


Hapendwi mtu, pesa kwanza wanaotususia shauri yao.
 
Mikopo ya kufanya nini ? Na sisi ni Lini tutawapa Ufaransa Mikopo ? Tunashindwa kuelewa kwa wao kutupa mikopo kwao ndio Biashara; Na kuhusu Ruzuku kwanini watupe sisi wakati huko Paris kuna Slums zenye uhitaji pia....

 
1000212624.jpg
 
Back
Top Bottom