Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa watanzania kupata chanjo ya CORONA kwa kuwa tiba ya maradhi hayo hugharimu taifa
Pia amesema ukipata corona kupona au kufa ni hamsini kwa hamsini, na kuna uwezekano mkubwa wa mtu kufariki
Ametoa wito kwa watanzania ekupata chanjo ili kuepuka vifo
Kama mtoa Uzi hujamlisha maneno mama, basi wasaidizi wake wanaompa data za corona wajiuzulu kwa kumfedhehesha mbele ya umma kwa kumpa data za uongo!!
Mama anasema ukiugua korona kufa au kupona ni 50 kwa 50!! Maana yake ni kwamba kwa kila watu 100 waliougua corona 50 watakufa na 50 watapona!!
Ukweli ni kwamba kwa kila watu 100 watakaougua corona 80 hata hawatajua kama waliwahi kuugua corona. 13 watapata dalili nyepesi kama mafua, kikohozi, nk. 4 watapata dalili Kali kama kushindwa kupumua, homa Kali, nk na 3 ndio wanaweza kufariki!! Covid 19 sio miongoni mwa magonjwa 10 yanayouwa zaidi hata huko marekani ambako corona imeua kuliko nchi yoyote!!, Sababu ya kumpotosha mama ni ipi? Hatukubali kutuaibishia raid wetu, lazima watu wawajibike! Takwimu rasmi hadi Leo tarehe 18/10/2021 ni kama ifuatavyo:
1. Tanzania: walioambukizwa corona ni 26,034. Waliokufa ni 724. Kwa hiyo waliopona ni asilimia 97.22% na waliokufa ni asilimia 2.78%.
2. Marekani: Walioambukizwa ni 45,792,532 na waliokufa ni 744,546. Kwa hiyo waliopona ni asilimia 98.38% na waliokufa ni asilimia 1.62%.
3. Duniani kwa ujumla:
Walioambukizwa ni 241,546,207. Waliokufa ni 4,915,686. Kwa hiyo waliopona ni asilimia 97.96% na waliokufa ni asilimia 2.04%.
Hiyo 50 kwa 50 aliyosema mama kama kweli kasema imetoka wapi??
Kama mama kapotoshwa, halafu akachukulia poa na asimwajibishe mtu, watu watachukilia kuwa alikuwa na maslahi katika kupotoshwa huko na hiyo ni picha mbaya zaidi!!
Swali la msingi tusaidiane hapa: Je ni kweli mama kasema ni 50 kwa 50 kufa au kupona kwa ugonjwa was corona? Kama ni kweli je takwimu hizo kapewa au kapika mwenyewe? Kama kapewa je hatua gani imechukuliwa kwa waliomfedhehesha mbrle ya dunia? Kama kapika mwenyewe hizo data, je no kwa maslahi gani?