Pre GE2025 Rais Samia ukitaka upite uchaguzi 2025 komaa na kundi la vijana, kama Hayati Magufuli alivyochagua kundi la wanyonge

Pre GE2025 Rais Samia ukitaka upite uchaguzi 2025 komaa na kundi la vijana, kama Hayati Magufuli alivyochagua kundi la wanyonge

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ingekuwa kura zetu zinaamua nani kiongozi, wangetusikiliza.

Ila kwa kauli zao mbele ya umma, ambazo ziko on record, ikiwemo
  • Hata mumchague nani CCM itaunda serikali
  • Sisi na wajuzi wa kuiba kura, na kutubu baadaye
  • Kupita bila kupingwa ni jitihada zetu tulizofanyia porini
  • Ushindi mlioupata hata sisi tumo (huku afande akiweka ishara ya kushikilia mtutu wa bunduki)

Kuna haja gani ya kutusikiliza?

As long as hakuna consequences zozote viongozi wanapata kwa kuziba masikio, hakuna kitu kitaenda. Mfumo wa demokrasia unategemea consequence iwe kwenye uchaguzi. Hilo wameweka kwapani.

Sasa ni mwendo wa kuomba hisani.
 
Mama Atafika 2025 amechoka sana kwa mtazamo wangu.Ukimwona anavyoongea ni kama amekata tamaa kwani kwa sasa anaongelea matukio na sio mipango ya nchi.Pia naona waliomzunguka wanamdanganya hawamwambii ukweli kwa kuwa huku nje kundi la vijana ni kubwa ingawa huwa halipigi kura(au kama alivyosema wengine ,kura haziamui mshindi Tanzania) .After 2025 CCM isipoangalia itapata wakati mgumu sana kuongoza watu kwa kuwa sasa watu wana fedha chafu na kundi hilo dogo mkuu wa nchi asipoangalia litamtesa sana.Mwenyekiti wa CCM ,atapata wakati mgumu sana kwa mtazamo wangu kuyadhibiti makundi ndani ya CCM na hasa vijana walioshawishiwa au kuona kuingia CCM wataula na kuambulia patupo(wanaokula fedha ndefu ni wenye network tangu zamani).Vijana wanabaki wakipelekwa kwenye ajira za kulipwa shs 600k kwa mwezi wakijua ajira ni mkombozi .Mambo ni mengi nimeyaona ,ila tusubiri 2025.
 
Ingekuwa kura zetu zinaamua nani kiongozi, wangetusikiliza.

Ila kwa kauli zao mbele ya umma, ambazo ziko on record, ikiwemo
  • Hata mumchague nani CCM itaunda serikali
  • Sisi na wajuzi wa kuiba kura, na kutubu baadaye
  • Kupita bila kupingwa ni jitihada zetu tulizofanyia porini
  • Ushindi mlioupata hata sisi tumo (huku afande akiweka ishara ya kushikilia mtutu wa bunduki)

Kuna haja gani ya kutusikiliza?

As long as hakuna consequences zozote viongozi wanapata kwa kuziba masikio, hakuna kitu kitaenda. Mfumo wa demokrasia unategemea consequence iwe kwenye uchaguzi. Hilo wameweka kwapani.

Sasa ni mwendo wa kuomba hisani.
Asante kwa uchangiaji,

Ukweli ni huu, hakuna serikali yeyote duniani iliyopo madarakani bila mapenzi ya wananchi,
Bado najaribu kutafakari mnalazimisha kitu gani enyi waja.

Haja ya kutusikiliza ipo kwa vile sisi vijana hatuoni furaha kuishi na changamoto, changamoto sio sifa ingawaje hakuna maisha bila changamoto.

Muache Mama awasikilize vijana.
 
Back
Top Bottom