Ingekuwa kura zetu zinaamua nani kiongozi, wangetusikiliza.
Ila kwa kauli zao mbele ya umma, ambazo ziko on record, ikiwemo
- Hata mumchague nani CCM itaunda serikali
- Sisi na wajuzi wa kuiba kura, na kutubu baadaye
- Kupita bila kupingwa ni jitihada zetu tulizofanyia porini
- Ushindi mlioupata hata sisi tumo (huku afande akiweka ishara ya kushikilia mtutu wa bunduki)
Kuna haja gani ya kutusikiliza?
As long as hakuna consequences zozote viongozi wanapata kwa kuziba masikio, hakuna kitu kitaenda. Mfumo wa demokrasia unategemea consequence iwe kwenye uchaguzi. Hilo wameweka kwapani.
Sasa ni mwendo wa kuomba hisani.