Rais Samia: Ukiwa nje ya Serikali unaona mambo ni rahisi, ukiingia mambo ni magumu

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
12,213
Reaction score
28,916
"Nimesikia watu huko kwenye mitandao wanalalamika kuwa nachukua watu hodari na kuwaingiza Serikalini kuwa naua sekta binafsi lengo sio kuua tunataka kuchanganya na kupata ubora maana ukiwa nje unaona huku Serikalini ni mambo ni rahisi lakini ukiingia unakuta magumu sana," alisema Rais Samia.

Hii inamaanisha kuwa Rais mwenyewe alipokuwa Makamu aliona vitu ni Rais sasa anaonja joto la jiwe.

Hapa pia anawaambia wapinzani kuwa wasifikiri kuongoza ni rahisi wasitegemee siku wakishinda mambo ni rahisi, kuongoza nchi sio jambo dogo.

USSR
 
Hapa pia anawaambia wapinzani kuwa wasifikiri kuongoza ni rahisi wasitegemee siku wakishinda mambo ni rahisi, kuongoza nchi sio jambo dogo
Acheni mikwara nyie......hakuna ugumu wowote ule.
 
Ni ngumu sababu ya mifumo ya hovyo
 

Anasema kuongoza nchi sio kazi rahisi, lakini unakuta wanapora uchaguzi ili kuendelea kukaa madarakani kwa shuruti.
 
Tatizo mama anadhulula sana hivyo kuwapa nafasi vijana wake wapigaji...anaacha kapanga ili akija kurudi toka alipokimbilia kula bata anarudi anakuta washaharibu....Atulie kama mtangulizi wake mzee kidevu mbona nchi ilikuwa inasonga tu?!
 
Kwa hiyo 2025 tutapata uchaguzi huru na wa haki ili kuthibitisha kama kuwa Rais ni kazi ngumu sio ya kuipata kwa kupora?

Ma CCM usiwaamini wanapenda mno madaraka,maneno yake ni hadaa tu

Hawapo tayari kuachia madaraka hawa
 
Kwa Katiba hii ya sasa haihitaji uhodari wowote ili kuendesha Nchi hii, unatakiwa uwe na PhD kwenye uongo majungu na tumbo kubwa lisilojaa.
 
Kama ameshindwa akae pembeni mapema kabla mambo hayajaharibika zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…