Rais Samia: Ukiwa nje ya Serikali unaona mambo ni rahisi, ukiingia mambo ni magumu

Maana gani
 
Tatizo kubwa kuliko yote ni ubaya wa katiba yetu. Fikiria sheria inayomlazimisha Rais ateue mawaziri kutoka kwenye kundi la wabunge, huku ikifahamika wazi hao wabunge wa sasa wote walipachikwa na marehemu kwa kukidhi sifa mbili kubwa aliyoipenda marehemu: kumsifia, na kutohoji chochote ambacho ameamua kufanya.

Katiba mpya pendekezwa ya Warioba ilitaka mawaziri wasiwe wabunge. Maana yake Rais awe na uwezo wa kumteua mtu yeyote miongoni mwa Watanzania, anayeona ana uwezo. Kabla ya mabadiliko ya katiba, hapo mwanzo ndivyo ilivyokuwa, mawaziri hawakuwa wabunge. Kwanza hiyo ingewaondoa wale wote wanaogombea ubunge kwa nia ya kuvizia uwaziri.
 
Acha uongo sio lazima rais kuteuwa mawaziri kwenye Wabunge, Rais amepewa nafasi kumi za uteuzi Hivyo anaweza teua mtu akaampa ubunge then uwaziri,hata Magufuli aliwapa uwaziri akina Kabudi,Mpango,Ndalichako nk,pasipo kuwa Wabunge wa majimbo.
 
Kwa Katiba hii ya sasa haihitaji uhodari wowote ili kuendesha Nchi hii, unatakiwa uwe na PhD kwenye uongo majungu na tumbo kubwa lisilojaa.
Auu....Alimaanisha Uhodari katika kulamba Asali Mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…