Rais Samia: Ulaya na Marekani hawafanyi vizuri kiuchumi kama sisi

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Rais Samia, amesema kwamba licha ya hali tete inayoikumba dunia kwa sasa, Tanzania inafanya vizuri kwa viwango vya kuvutia kiuchumi. Akiwahutubia wananchi wa Simiyu katika ziara yake ya kikazi, Rais Samia alieleza kwa msisitizo hali halisi ya ulimwengu na nafasi ya Tanzania ndani yake:

'Ukitegemea msaada wale wanaotoa msaada dunia yote sasa ipo juu chini. Mavita, maugomvi, mavurugu, chumi zimeshuka, huko hawafanyi vizuri kama tunavyofanya sisi.''

Katika kauli hiyo, Rais Samia aliweka bayana kuwa hata mataifa makubwa yanayojulikana kwa nguvu zao za kiuchumi hayako tena katika nafasi ya kuigwa kwa sasa

''Ulaya na Marekani sasa hivi hawafanyi vizuri kiuchumi kama tunavyofanya sisi huku, hata ndani ya kanda yetu hii ya Afrika Mashariki, Tanzania tunafanya vizuri.”

Your browser is not able to display this video.
 
Naona Aibu mimi kuongozwa na muhudumu wa ndege.

Mlevi alipelekwa mahakamani kwa kosa la kutukana ovyo
Hakimu : "wewe mbona mara kwa mara unaletwa hapa"
Mlevi : "Mbona na wewe kila siku nakukuta hapa na sikwambii kitu"
 
Ngoja ninyamaze, dunia simama nitelemke! Tumepatikana ......................
 
Haya mambo sometimes bora asiyaongee inachafua image yake in publick
 
Hivi kawachukuliaje wananchi wa Simiyu😅
 
Da na yale mataputapu yakaunga mkono na yakasema!! Mitano tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…