Michelle
JF-Expert Member
- Nov 16, 2010
- 7,628
- 3,535
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Amiri Jeshi Mkuu na Mwenyekiti wa Chama tawala Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mheshimiwa Rais Pole kwa majukumu mengi sana.
Nikupongeze kwa kujitahidi kuifanya kazi uliyoapa kuifanya kadri ya uwezo wako.
Mheshimiwa Rais baada ya kuapishwa uliupa taarifa umma wa watanzania waliokuwa na huzuni na wengine matumaini kidogo kuwa wewe ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwenye jinsia ya kike. Wenye akili zetu za kiasi,tulikuelewa na tulitaka usimame hivyo hivyo. Ukatushangaza wengi ulipoanza sasa kuondoka kwenye msimamo huo wa kijasiri kwenda kuwa Mama. Na vijana kwa kujua unapenda nafasi hiyo sana na wao wakajiita chawa wa Mama,Vijana wa Mama Kizimkazi,Vijana wa Samia na Watoto wa Mama. Chawa wakawa na jeuri ya kufanya yaliyokupendeza na mengine ambayo hayapendezi kwa viongozi wengine. Lakini uchawa ukaendelea na umekuwa mkubwa na sasa wapo wanaotaka kuongoza chawa na kuwa chawa wakuu na wa kipekee. Majina na vyeo vya chawa yanatofautiana ila kazi yao ni ile ile.
Mheshimiwa Rais: Ni wakati sasa kusimama kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri jeshi mkuu. Huna watoto nje wale wa kwako. Hawa watoto wengine ni watoto maslahi,wanakutazama kama fursa ya kufikia malengo yao. Si jambo baya,riziki zetu hupita mikononi na midomoni mwa watu. Kosa ni pale unapojiona huna watu na kuamua kuchukua yule anayepatikana kwa wakati huo mwenye ujasiri wa kufanya yale ambayo watoto wako usingeruhusu wafanye. Katika yote yanayoendelea nchini kuna jambo moja tu ambalo linasumbua utawala wako na linalosikika zaidi: RAIS HANA UJASIRI. Mheshimiwa Rais kuna mengi mezani kwako,usikwepe kuyashughulikia,shughulikia matatizo ya watanzania yaliyoko mbele yako: Bima ya Afya,NSSF,Maafa ambayo pamoja na kuundiwa kitengo bado hatujaweza kujiandaa na kukabiliana nayo,ripoti ya CAG,ubadhirifu wa mali za umma na fedha za umma,shughulikia mienendo ya mawaziri na wasaidizi wako isiyokubalika kwenye jamii na tafuta diplomasia ya kushughulikia matatizo ya ardhi nchi hii na hasa yanayohusisha uwekezaji.
Nakupa taarifa unayoifahamu,hakuna anayekuhurumia,kwenye nafasi uliyo nayo huruma,jinsia yako na kujitolea kuwapenda watoto ambao wengine upendo ni utumwa ni vile basi tu tufanyeje sasa, hakutakupa huruma,watu wanataka maisha bora kwao na familia zao.
Tanzania ni nchi pekee ambayo wengi wetu tuko mitandaoni muda mwingi sana,ukijifanyia tathmini ya kukubalika kwako kupitia kwa social media addicts wakiongozwa na chawa utaamini unakwenda vizuri na pengine watakushawishi hivyo,Mh. Rais hali sivyo ilivyo kwa watanzania Milioni 50 huko. Usidanganyike na vipicha picha na graphics nzuri nzuri zinazozungushwa,maumivu kwa wengi wetu ni makali sana ya maisha. Na ni matusi kwetu na ndimu kwenye kidonda kuona misururu ya magari,matumizi yasiyo ya lazima ya serikali yasiyogusa hata shida za watanzania milioni 30 tu yakiendelea kupewa kipaumbele. Katika taifa ambalo wakinamama bado wanajifungulia chini ukiwaeleza majority ya watanzania wanaosikia shirika la ndege halipati faida kivile sababu za ndege kuongezeka hutaeleweka kamwe.
Mheshimiwa Rais: Ninayoandika una uwezo nayo,nikitazama DP World na maamuzi mengine ya awamu hii ya sita ninajua una uwezo wa maamuzi magumu na pengine yanayokwenda kinyume na wengi. Ni wakati sasa ufanye maamuzi magumu kwenye yale yanayoumiza maisha ya watanzania walio wengi. Simamia haki kwa vitendo,wajibisha wabadhirifu,kemea unayoyaona hayafai dhidi yako na viongozi wengine wote kama Chongolo na onyesha mfano kama Rais kwa kukemea na kudhibiti haya. Sisi tulisema humu kuwa ya Chongolo yataendelea na sasa matokeo yanaonekana. Sioni chawa wakikutetea sasa,kwasababu pengine viposho haviwatoshi au mgao haujawafikia. No free lunch dunia hii na kwakuwa hawana cause wayoipigania zaidi ya kula yao,hawajisumbui.
Mheshimiwa Rais: Nimalizie kwa kuzungumzia yanayoendelea kuzungumzwa juu yako na Mange. Kuna wakati huwa najiuliza hata ingekuwa kweli yanayosemwa,ni kwa namna gani yanaathiri utendaji kazi wako? Historia haitufundishi kuwa dunia imekuwa na wanasiasa perfect maana hata kina Obama wana tuhuma za aina hii. Sikuwahi kusikia wasaidizi wa Rais Obama wakimuita 'Daddy yao' na kutishia watu juu ya tuhuma za Obama mbele ya Rais Obama na viongozi wakuu kwenye tukio la IBADA ya kumuenzi kiongozi aliyepumzika. Najiuliza sana,ni nani aliruhusu haya na lengo likiwa nini kwenye nchi ambayo ina vyombo huru,viongozi kama Makonda wanaweza kwenda kuongelea popote? Kwa nini ukubali unyonge? Kwanini vyombo vyako vinakubali unyonge wa kushindwa kuchukua hatua hadi mkuu wa mkoa ajitoe kufanya kazi yao? Kwanini mamlaka zinazoshughulikia maadili ya viongozi havitaharifiwi na kuchukua hatua dhidi ya wanaotuhumiwa au kuhisiwa? Mh. Rais kuwa makini na isolation strategy inayotumika dhidi yako. Utabaki na mtoto wako wa kipekee na atakaa kwenye kiti unachotaka kuendelea kukaa. Sisi wanawake tuliozoea kupitishwa kwenye moto tunakushauri kataa unyonge,kataa kupendwa ukihadaiwa,kataa sifa za kijinga na kishamba na mwisho kabisa kataa kupuuzwa. Nimesikia Lema akisema wakupe kadi ya CHADEMA,kwa maoni yangu hapatakuwa na Lowassa mwingine hivi karibuni,zile ni kejeli. Zipuuze na fanya yale watanzania wapambanaji wanayotaka ufanye kwa manufaa ya wengi. Huna chama kingine cha kwenda,maliza mwendo kijasiri na kibabe kabisa,historia ikukumbuke vyema. Tupe na Katiba bora,waache watanzania waamue wanavyotaka kujiongoza na kuongozwa,acha legacy nyingine tofauti na ile ya kumalizia miradi uliyoikuta,malizia na mabadiliko ya katiba ambayo hayakutimia ila watanzania wanayahitaji. Na anza na kuondoa viti maalum,huo nao ni unyonge. Twende tukapambane,tukishindwa tutajifunza pa kuanzia next time.
Kazi Ianze muda wa kujifunza umeisha. Unaweza,twende kazi sasa.