Rais Samia ulishangiliwa, lakini ubora wa jukwaani haufurahishi

Rais Samia ulishangiliwa, lakini ubora wa jukwaani haufurahishi

robinson crusoe

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2020
Posts
762
Reaction score
1,236
Kwa mara nyingine tena tukubali kwamba Tanzania hatujaweza kuwa na mchujo wa kupata viongozi wenye busara. Busara hutokana na kuiga pamoja na uzoefu. Kwa mtu aliyeweza kuwa kiongozi wa nchi haistahili awe na mapungufu ya kiwango hiki. Yaani sasa rais ameamua kuja majukwaani na washangiliaji wenye nguo za kijani.

Rais anakuja kuhutubia mambo ya uchumi wa kitaifa akiwa na washangiliaji binfasi. Kwa ujumla rais Samia ameonesha udhaifu wake halisia ktk uongozi.

Baada ya Mh. Ndugai 'kumkosea'na baadaye akaomba msamaha wa wazi, imekuwa ni aibu kumuona rais wa nchi (siyo kijana mpiga mdundiko) akijitokeza na kuanza kujibu mapigo na kujigamba uwezo wake, na kutoa ahadi ya kuwaondoa watu madarakani.

Je, kwa tabia hii Samia anaamini ameonesha ushujaa? Kiuongozi, huku ni kupwaya! Ni kuonesha uwezo mdogo na washauri wake ni wa uwezo mdogo.
 
Tanzania ni nchi ngumu Sana.....unaweza kukonda kwa siku 2 tu ......Sijui Kama mataifa mengine yapo Kama Tz.......

Anyway ......wajuzi mnipe majibu
 
Acheni mfumodume ni wa kijinga kabisa na haukubaliki
Magufuli alibeba wanamuziki kina Diamond Kiba Zuchu hamkumuona
Leo kimewauma wenyeviti wa CCM wa Mkoa na Wakuu wa mikoa waliokuja kusikiliza majumuisho ya mkopo Acheni wivu wa kisukuma na wa wagogo wanaowadharau wanawake
 
Back
Top Bottom