Rais Samia umeanza Vyema, Malizia ng'we iliyobaki, tunakupongeza

KISHADA

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
2,226
Reaction score
3,291
Binafsi nakupongeza sana kwa namna ulivyoanza na namna unavyoendelea kuipigania nchi yetu kusonga mbele.

Kwa uchache wa maneno umejitahidi katika maeneo haya muhimu.

Umejitahidi kuifungua nchi yetu kidiplomasia na kujaribu kuirejesha sehemu yake inapostahili. Tumeona jitihada zako za kwenda huku na kule, tumeona speech zako popote upatapo fursa, tumeona vitendo vyako na moyo wako unavyoguswa kuhakikisha Tanzania inarudisha imani kwa jumuiya za kimataifa na kujenga mafungamano. Naamini ulijua kosa liko wapi na sasa unajaribu kulitibu. Tusifukue yaliyopita ila Tanzania haikupaswa kwenda mwenendo ule si haba hili umeliona na umelifanyia kazi.

Umeanza vyema kurudisha imani na mshikamano wa watanzania. Tulikua na hali mbaya ambayo ilifichwa kusemwa. Mwenendo wa kisiasa, mshikamano wetu haukuwa ule tuliouzowea. Paliingia fitina kubwa na mivurugano iliyopata baraka za kidola. Hatua ulizoanza ni nzuri.

Kwanza kukaribisha watu kukutana na kuzungumza, kufungua milango ya uwazi na habari iliyofungwa kwa muda, kusafisha wale ambao walionekana kikwazo. Lakini ngoja nikwambie hapa. Bado kazi iendelee hapa maana kumejaa mabaki, wengine watajificha baada ya kuona mwenendo wako wafichue.

Kuna kazi ya kusafisha mifumo yetu ya utoaji haki, mifumo ya upelelezi na kubambikizia, mifumo ya kulindana n.k. Mama jitahidi sana kuwabaini wale ambao wanadhani walistahili kuendeleza vitendo vyao vya dhulma lakini kwa sasa wanahaha kujificha, wabaini wasijekukuharibia maana hawakuridhika na haya unayoyafanya.

MALIZIA NG'WE ILIYOBAKI
Jitahidi mama yetu haya yafuatayo ukiona inafaa kwa njia sahihi.

Fumua sheria zote kandamizi zilizotungwa ambazo hazijengi mustawa mwema wa Taifa, naamini ziko nyingi unazijua, nenda taratibu utafanikiwa, Sheria za Habari, Sheria za Chaguzi, Sheria za kodi n.k. Angalia mapungufu na fumua, bakisha mazuri tu.

Fungua dirisha la demokrasia lililofungwa, Ongeza juhudi tena hapa, ulianza vyema kwa hutuba za matumaini sana jitahidi kuonesha vitendo zaidi, yale maneno ya pale TCD ni msingi sasa weka tofali.

Ongeza juhudi za uwazi na habari, ruhusu makongamano ya mada za kitaifa na ushirikishawaji wa wadau.

Ki- "shape" Chama chako na jumuiya zake kukumbatia dhana sahihi ya demokrasia ya vyama vingi. Ushindani wa sera na kujitegemea na si kutegemea Dola. Tumia vipaji vya vijana wa chama na wazee wazoefu kuitengeneza siasa yetu na mustakbali wa nchi yetu kwenye misingi yake ya uasisi. Huko kwenye chama ndiko kwenye shina la Tanzania tuitakayo. Somo la Demokrasia ya vyama vingi lipelekwe chamani maana huku hatujafanya vizuri. Vijana waache kudeka, wabuni miradi na kujitoa kufanya kazi.

Fumua mifumo ya utoaji haki iwe wazi na inayoaminika. Hili ni eneo lililoathirika, jitahidi kuhakikisha haki za watu zinapatikana kwa wakati. Wewe ni muumini wa sheria na haki, hatuna wasi wasi. Jiridhishe usije kudangwanywa kisheria sheria maana watu ni mafundi kwa kazi zao ili wasije kukuharibia hao walimwengu.

Mama kuna hili la Haki za wafanyakazi na stahiki zao. Hapa mama malizia kazi uliyoianza. Malizia kada zote zilizobaki wakimwemo watumishi wa Umma wa kawaida. Hili kundi linahitaji kuponywa hasa. Umeanza vyema jitahidi kumalizia hatua iliyobaki. Usisahau haki za wastaafu na makundi maalumu kama ilivyo dhamira yako.

Kuna Katiba mpya ambayo tunasubiri maelekezo yako baada ya kuangalia muda sahihi.

Kipato na hali za maisha za mtu mmoja mmoja huko mitaani

HITIMISHO
Mambo ni mengi yengine sijayataja kutokana na muda. Tunakupongeza kwa dhati na tunaamini kuna mambo yanakusononesha. Umeanza vyema sana na tuna imani unayajua matarajio ya watanzania wengi.

Watu walishusha pumzi mara tu ulipoingia madarakani nadhani hili linakujia kila wakati. Imani hio inapaswa kumaliziwa kwa Spirit ile ile na naamini kuna mahala umekusudia kutupeleka. Yote kwa yote tunakupongeza kwa namna ulivyoanza na tunakuombea kwa Mungu akupe uwezo zaidi wa kuyasimamia hasa yale mambo yenye uhusiano na ujenzi wa mshikamano wetu, uchumi wetu na udugu wetu.

Kishada
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣😃
Yaani hiiiiiiiiiiiiiii,mwenzetu hata inlation haikupi shida.
 
Tutatumia dola kuingia ikulu.......stupid Bashiru
 
Back
Top Bottom