Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Mhe. Rais ameiambia Dunia kwamba Freman Mbowe amekamatwa na Jeshi la Polisi baada ya kutoroka nchi mwaka 2020. Nakosa maneno mazuri yakukosoa kauli hii ila naomba nitumie busara kusema si maneno sahihi ya utetezi yaliyopaswa kutolewa na Mhe. Rais. Ni kauli inayodhihirisha wazi kwamba Mbowe anafunguliwa makosa ya ugaidi kwa maelekezo maalumu. Na naomba niunge mkono hoja yangu na ushahidi ufuatao.
Pia soma > Rais Samia: Mbowe alijificha Nairobi aliporudi akaanza harakati za katiba
1. Raia yoyote anayetaka kusafiri nje ya nchi lazima aruhusiwe na wanajeshi wa Uhamiaji ambao wapo kila mpaka. Bila ruhusa ya Askari wa Uhamiaji Tanzania kuruhusu mtu kuondoka nchini uwezi kuruhusiwa kuondoka na hata upande wa pili awawezi kukupokea. Ni ukweli ulio wazi kwamba Mhe. safari zake zote nje ufuata taratibu. Kama alitoroka Basi alitakiwa kushtakiwa kwa kuvuka mpaka kinyume Cha sheria.
2. Kama ilivyo kuondoka , kuingia nchini pia lazima upite kwenye dawati la wanajeshi wa Uhamiaji wakuruhusu kuingia nchini na yeye alifanya hivyo ndo maana hakuna shauri lililofunguliwa dhidi yake la kuingia nchini kinyume cha sheria.
3. Je, jeshi la Polisi na hao maafisa usalama kwanini awakumkamata wakati anatoka au kuingia?
4. Baada ya kuingia nchini alifanya Mikutano na vyombo vya habari, hakukamatwa. Alizunguka karibu nchi nzima kuzindua chadema digital hakuna aliyemkamata na haya yote yanafanyika Mhe. Rais akiwa madarakani.
5. Alipata msiba na akaenda msibani hakuna aliyemkamata.
6. Alisafiri kwenda Mwanza, RPC Mwanza alipohojiwa akasema amepokea maelekezo kutoka juu na hakusema Ugaidi.
7. Alitolewa mwanza akapelekwa Dsms ambapo RPC wa kinondoni alimweleza wazi kwamba atamfungulia makosa yasiyo na dhamana.
8. Rais anazungumzia CDM ambayo imesajiliwa na ipo kihalali as if siyo chama Cha siasa anachokitambua na kwa matamshi yake Ni Kama yeye anaamini chadema haipaswi kuwepo ila hatoi sababu kwanini isiwepo.
Kwa mazingira haya ni wazi kwamba mahakama inacheza ngoma za kisiasa na haya ndiyo yaliyofanywa na awamu iliyopita yakujaza watu Magereza bila hatia kisha JPM alipofariki tu Wana ccm wote wametolewa Magereza kwa kauli mbiu usirithi adui wa mwenzio. Je, tukiendelea na mfumo huu wa kila kiongozi kuelekeza kuwekwa ndani kwa mtu mwenye fikra tofauti na zake tutaligikisha pahali gani Taifa?