Rais Samia umedanganywa Mbowe alitoroka nchi ukakubali au umeamua kuruhusu utetezi wako kukosolewa?

Sikuwahi kumdhania mama kufikia hatua hii ktk maisha yangu, nilimsifia hadharani bila woga nikijua makosa yaliyofanyika na mtangulizi wake ya kubambika watu kesi na kuwatia magerezani yameisha kumbe wembe ni uleule kama wimbo wao wa kampeni za ccm unavyosema. Mama ataingia kwenye historia na kudhihirishia ulimwengu kuwa mwanamke hawezi madaraka makubwa kama vitabu vya Mungu vinavyosema. Ktk watu nilikuwa naamini ni washika dini na wenye hofu ya Mungu ni Wazanzibar ila kwa huyu mama basi.
 
Jeshi la polisi, jeshi la magereza, jeshi la mgambo, jeshi la uhamiaji, nk...
sawa.. hii ni kwa tafsiri yako binafsi, ila naomba urudi tena shule au muulize mzee yeyote atakuelewesha, manake nikikwambia uende library ni mtihani, na nikikwambia utumie mtandao kutafuta neno jeshi au kwa lugha ya malkia "military" itakuwa ni adhabu...
 
Uwongo mtupu jamani kha!
 
Ni kheri alivyokua kimya kuliko anayoyatamka sasa hivi
 
Ila Mungu fundi aiseee, ukisikiliza hio clip unaona kabisa ameshaanza kubanwa na Mafua makali hata sauti haitoki! Wacha nitafune ubuyu
Tayari Watu Wameanza Kusoma Surrat~Zubaa Na Ubani Mashtaka Huku Chumvi Ikimiminiwa Aliye Juu Ndiyo Hutoa Hukumu Sahihi
😀😁😂🤣😃😄😃😅😄😃
 
Usisahau pia alituma salamu ya pole kwa kufiwa na kaka yake?
 
Nilichoelewa.. Alisema anatibu kwanza majeraha.. LAKINI HAKUSEMA HAYO MAHERAHA YALISABABISHWA NA NANI..!! Naona kaamua kuweka majeraha yake..!!
 
Umejawa ubishi, kisa Dada kaandika jeshi la uhamiaji...

Kichwa chako kimeganda hakitaki kuelewa kuwa kuna

Jeshi la polisi
Jeshi la zimamoto
Jeshi la mgambo
Jeshi la magereza na mengineyo...

Ingia katika tovuti ukaone ukasome, sio sisi ni imeandikwa na kuelekezwa hivyo

Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama

Kichwa chako kimekuwa mgando una anza kifalu na kifaru...
 
Yaani mtu anayeshitakiwa kwa ugaidi
1. Amevuka mpaka kwenda Kenya
2. Akavuka mpaka kuingia/kurudi Tanzania
3. Amefanya mikutano kadhaa tena inawezekana mikutano mingine ilihusisha kuandika barua polisi
4. Amehudhuria msiba wa kaka yake na akapewa pole na Rais

HUYO GAIDI WA KUACHIWA AFANYE YOTE HAYO HUKU UPELELEZI UKIENDELEA NI GAIDI WA AINA GANI?

KWANINI HAKUKAMATWA TOKA WAKATI HUO NA HUKU MAGAIDI WENZIE WALIKUWA CHINI YA ULINZI, NA WENGINE RAIS KASEMA WAMESHAHUKUMIWA?
 

SSH na chama chake wanajua fika kwamba hawana tena uwezo wa kupambana kisiasa kwa hoja. Uchaguzi uliopita walipora kwa mtutu wa bunduki. Hata JPM aliwaambia wabunge wake kuwa hawakushinda uchaguzi. Yeye mwenyewe na "uchuma" wake wote alipiga magoti kuomba kura ingawa haikusaidia na kulaximika kupora uchaguzi. Kwenye kampeni SSH alikiri kuwa wanakwenda kupora uchaguzi! Wamejiuliza huko mbele ya safari wataendelea kufanya kupora uchaguzi? Labda; lakini mbali ya hilo lazima upinzani uhujumiwe kwa kumuondoa kinara wa siasa za upinzani. Wamefilisika kupita maelezo. Kuendelea kuongozwa na wanasiasa mbilikimo kiasi hiki ni kuchelewesha maendeleo yake.
 
Tatizo la watanzania kila mtu ni Polisi, utamkamataje mtu wakati upelelezi haujakamilika?? Hata kama upelelezi ulikamilika namna ya kumkamata mtuhumiwa ni taaluma pia.....kama huna uelewa wa mambo yaache kama yalivyo wafanye watu waliosomea na wenye taaluma na hizo vitu.

Mtu from nowhere anasema mbowe gaidi! Ukimuuliza afafanue kwanini mbowe sio gaidi hajui! Watu hata hawajui ugaidi na viashiria vyake halaf anakurupuka kuongea upuuzi tu.
 
Huyo Gaidi Mbowe ana kesi ya ugaidi tangu mwaka jana ilikuwa inapelelezwa hivyo mwaka huu upelelezi umekamilika tena wamemsaidia tu alitakiwa awe ndani kama wenzake waliokuwa ndani tangu mwaka jana. Kwanini mnamtetea Gaidi Mbowe tu na wala si wale chadema wenzenu magaidi yaliyokamatwa tangu mwaka jana? Ndiyo maana magaidi menzake yameamua kusema kila kitu ili wafungwe wote.
 
Nimeikumbuka kauli yake ya mimi na Magufuli ni kitu kimoja
 

Kwani wewe Shida yako hasa Nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…