Rais Samia Umetubadilishia Mkurugenzi wa EWURA, tubadilishie na wa TPDC na PURA

Rais Samia Umetubadilishia Mkurugenzi wa EWURA, tubadilishie na wa TPDC na PURA

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Nimeyazungumzia haya mashirika mawili yanayohusika na uendelezaji wa mafuta na gesi Tanzania.

Tunaomba tubadilishie wakurugenzi wa hayo mashirika tuone mabadiliko katika sekta ya mafuta na gesi.

Wakurugenzi wanakaa kwa muda mrefu sana, hapo inaweza kuwa ngumu kuona mabadiliko.

Zoezi la kubadilishana uzoefu ni zuri sana ili kuleta mawazo, maarifa na uzoefu mpya katika shirika.

Kubadilishana sio jambo baya, katika taifa letu. Tangu harakati za kutafuta gesi na mafuta kwa kasi zinaanza Tanzania tumekua tukiwasikia wakurugenzi walewale.

Leo ni 2023, gesi haijasambazwa vya kutosha kwa watanzania. Ukiangalia idadi ya watanzania wanaotumia gesi asilia Dar es Salaam haifiki hata 1000 ukilinganisha na idadi ya wakazi milioni 8 wanaoishi Dar es Salaam.

Gesi utilization plan haijatumiwa ipasavyo: Plan ilisema tutakua na viwanda mbalimbali vitakavyotumia gesi kama malighafi kuzalisha bidhaa.

Mfano plan ya kiwanda cha Mbolea kilichopangwa kujengwa LINDI mpaka leo hakijajengwa. Tulikua na plan ya kusambaza gesi mikoani, mfano kuna wateja wengi wa gesi ARUSHA, MWANZA, na DODOMA. Ni kipi kimezuia kuipeleka gesi katika mikoa hiyo kama tuliweza kuileta Dar es Salaam.

Nitaileta gesi utilization plan ili tujisomee.
 
Back
Top Bottom