Rais Samia, una taarifa za changamoto ya mifumo ya TEHAMA nchini hasa kukosekana kwa huduma ya malipo up (control number)?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Ni takribani mwezi Sasa malipo ya serikali hayafanyiki kwenye taasisi mbalimbali baada ya kile kinachodaiwa mfumo wa hazina unaotoa control number kushindwa kufanya hivyo. Kutokana na changamoto ya control number fedha lazima zitakuwa zinapigwa kwa sababu huduma zinatolewa manually kitu ambacho Tulitangaziwa na Wizara ya fedha kimekwisha. Nimekwenda taasisi moja kuomba huduma nimekwamishwa na baada yakuwakomalia wakasema tatizo lipo nchi nzima.

Tatizo hili linatajwa kuchangiwa na wakandarasi wa mifumo yetu wasio Wazalendo na wasio na utaalamu wakutosha kufanya majukumu yao. Haiwezekani taasisi imalize wiki au wiki mbili haina internet au uwezo wa kutoa control number na hakuna taarifa kwa umma. Tutaamini vipi kwamba manualy way of payment pesa zinakwenda serikalini? Je,taasisi ambazo zimesitisha kutoa huduma kwa wateja wamekujulisha au wamekaa kimya wakisubiri uwazingue?

Walianza Tqnesco, watu wakapiga kelele mkarekebisha. Sasa hivi wamehamia taasisi nyingine zinazotoa huduma kwa control number. Waziri wa fedha amekaa kimya na Waziri wa mawasiliano amekaa kimya hadi watu walalamike ndipo waondoke ofisini wakajidai kutumbua watu.

Nisingependa kutaja taasisi zinazolalamikiwa kukosa huduma lakini naamini ukiomba status ya taasisi utaelewa ninachosema hapa. Watu wameanza kufanya kazi wanavyojisikia.( Wizara ya fedha, maliasili, Kazi, bandari, mambo ya ndani, elimu, afya na uchukuzi hali si shwari kwenye huduma wanatoa manually kinyume na matakwa ya maelekezo yako yakurahisha huduma na kutumia tehama). Watu wanalalamika kuchelewa kwa huduma

Jambo la pili ni ubadhirifu unaofanywa na mitandao ya simu kwenye matumizi ya bando. Unanunua GB 1 kwa wiki unatumia siku moja au mbili bando limeisha na hakuna adhabu inayotolewa kwa Vodacom, tigo, Airtel, ttcl kwa wizi unaendelea. Hadi wananchi tuseme ndo watachukua hatua,. Wizara ya mawasiliano waombe taarifa ya malalamiko ya wateja kwenye makampuni ya simu waone ukubwa tatizo, wanaiba bila hata kuona aibu.

Tatu, ttcl ni shirika la Tqifa ila linakwenda kufa, kukosekana kwa hizi huduma serikalini zinachangiwa na TTCl kushindwa kutoa huduma. Je, Mhe. Rais hakuna watendaji TTCl wanapata kiasi flani Cha gawio kutoka makampuni ya simu ili wahujumu shirika then uwape tenda makampuni hayo? Je, waendeshaji w ttcl wana vigezo?

Naomba kuwasilisha haya yasemwayo na wananchi kwenye mitandao, na mengine tunayojionea wenyewe.
 
Wizara ya Fedha kuongozwa na Mwigulu ni definite failure kwa rais.
Muda utasema
 
Wizara imepewa Dr wa binadamu hajui A,B,C za technology na mifumo ya mawasiliano. Ukimsikiliza tu unajua hajui anachokiongea. Hii wizara kwanza ipewe mtu mwenye uelewa ili hata waandamizi wakijifanya kumpiga chenga anaelewa mifumo na hadanganyiki
 
Alipatakina mtu aliyesimamia haya mkampiga Vita mpaka kafa. Sasa turudini Kule tulipotoka
Kinacho fanyika lazima kutakuwa na Mafisadi wanachezea hii mifumo ili baadhi ya malipo yawe yanaingia kwenye akaunti binafsi. Haiwezekani Gafa mifumo ya malipo isumbue. Lazima kutakua ja jambo linabafilishwa.


Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Nadhani Kati ya kipindi ambacho Wizara ya mawasiliano inatakiwa na mtu mfuatiaji wa mambo nikipindi hiki Cha serikali kutumia TEHAMA. Hapa Kuna uvamizi mkubwa kutoka ndani na nje kupitia uhalifu wa mitandao. Bila kuweka Waziri na katibu Mkuu anayezungumza lugha ya tehama tutapigwa sana.

Lakini pia lazima kwenye TEHAMA upunguze vulnerability ya mifumo, walioaminiwa ndio Wapewe haki yakusimamia na kutumia mifumo. Viongozi waandamizi wengi wa serikali hata kufungua email sidhani kama wanaweza. Na hao ndio wamekabidhiwa mifumo wasimamie. Do we think tutatoboa? Ujuzi na uelewa wa mifumo siyo jukumu la wataalam wa tehama nijukumu la viongozi wote wa taasisi katika ngazi zote.

Tehama inahitaji rasilimali, je wanapewa rasilimali? Kitendo Cha mifumo kusumbua Ni matokeo ya kuwa na watoa maamuzi wasioipa mifumo kipaombele. Na Kama ipo taasisi ina wiki mfumo unasumbua basi menejimenti yote ifekwe ili taasisi nyingine zielewe kwamba Tehama nikipaombele Cha Taifa.

Kuhusu Wizara ya fedha, huko Kuna tatizo kubwa. Waliokaa huko wengi wanalipwa vizuri na wameshiba hivyo nivigumu kufuatilia mianya ya upotevu wa mapato au kufuatilia ubovu wa miundomsingi ya utoaji huduma. Wanasubiri ripoti ya CAG tu,

Niombe sana tusikubali tukarudi kwenye urasimu wa kwenda ofisi za umma kupanga foleni na kukatiwa risiti zakuandika kwa mkono, tulipotoka tuliumizwa sana. Mhe. Rais wasimamie waliopo chini yako wafanye kazi kuilinda na kuboresha mifumo ya huduma.

Wawekezaji watakimbia kwa sababu tu ya urasimu wa kupata huduma na rushwa itaongezeka.
 
Kwa kweli hii ni Balaam hawa wasimamiaji wajiongeze.
Wana dukua vitendea kazi vya mapato.
TRA mpo, Wizard Fedha mpo mnapokea mishahara.
Mh Rais hili usilifumbie macho kuwa shubiri. Wajibisha mtu ili watendaji wajiongeze.
Watakuangusha vibaya!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…