Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Ni takribani mwezi Sasa malipo ya serikali hayafanyiki kwenye taasisi mbalimbali baada ya kile kinachodaiwa mfumo wa hazina unaotoa control number kushindwa kufanya hivyo. Kutokana na changamoto ya control number fedha lazima zitakuwa zinapigwa kwa sababu huduma zinatolewa manually kitu ambacho Tulitangaziwa na Wizara ya fedha kimekwisha. Nimekwenda taasisi moja kuomba huduma nimekwamishwa na baada yakuwakomalia wakasema tatizo lipo nchi nzima.
Tatizo hili linatajwa kuchangiwa na wakandarasi wa mifumo yetu wasio Wazalendo na wasio na utaalamu wakutosha kufanya majukumu yao. Haiwezekani taasisi imalize wiki au wiki mbili haina internet au uwezo wa kutoa control number na hakuna taarifa kwa umma. Tutaamini vipi kwamba manualy way of payment pesa zinakwenda serikalini? Je,taasisi ambazo zimesitisha kutoa huduma kwa wateja wamekujulisha au wamekaa kimya wakisubiri uwazingue?
Walianza Tqnesco, watu wakapiga kelele mkarekebisha. Sasa hivi wamehamia taasisi nyingine zinazotoa huduma kwa control number. Waziri wa fedha amekaa kimya na Waziri wa mawasiliano amekaa kimya hadi watu walalamike ndipo waondoke ofisini wakajidai kutumbua watu.
Nisingependa kutaja taasisi zinazolalamikiwa kukosa huduma lakini naamini ukiomba status ya taasisi utaelewa ninachosema hapa. Watu wameanza kufanya kazi wanavyojisikia.( Wizara ya fedha, maliasili, Kazi, bandari, mambo ya ndani, elimu, afya na uchukuzi hali si shwari kwenye huduma wanatoa manually kinyume na matakwa ya maelekezo yako yakurahisha huduma na kutumia tehama). Watu wanalalamika kuchelewa kwa huduma
Jambo la pili ni ubadhirifu unaofanywa na mitandao ya simu kwenye matumizi ya bando. Unanunua GB 1 kwa wiki unatumia siku moja au mbili bando limeisha na hakuna adhabu inayotolewa kwa Vodacom, tigo, Airtel, ttcl kwa wizi unaendelea. Hadi wananchi tuseme ndo watachukua hatua,. Wizara ya mawasiliano waombe taarifa ya malalamiko ya wateja kwenye makampuni ya simu waone ukubwa tatizo, wanaiba bila hata kuona aibu.
Tatu, ttcl ni shirika la Tqifa ila linakwenda kufa, kukosekana kwa hizi huduma serikalini zinachangiwa na TTCl kushindwa kutoa huduma. Je, Mhe. Rais hakuna watendaji TTCl wanapata kiasi flani Cha gawio kutoka makampuni ya simu ili wahujumu shirika then uwape tenda makampuni hayo? Je, waendeshaji w ttcl wana vigezo?
Naomba kuwasilisha haya yasemwayo na wananchi kwenye mitandao, na mengine tunayojionea wenyewe.