Leo nawaletea tena kituko kingine ambapo Samia amekiambia kile kikosi chake cha masuala yake ya demokrasia anayoitaka yeye kuwa yupo kwenye kiti cha urais hadi 2030.
Hivi vituko kwa sasa ni vingi sana na vinanichanganya kwa sababu ndugu zangu inajulikana kuwa mwaka 2025 kutakuwa na uchaguzi mkuu.Sasa Samia kajulia wapi sasa hivi kuwa atashinda uchaguzi huo?
Hiki kiburi cha hawa viongozi kuwaona Watanzania ni takataka wasiweza kuchambua mambo wanakitoa wapi?Nani kamwakikishia Samia kuwa atashinda katika uchaguzi mkuu wa 2025?
Tanzania tutaendelea kuwa na viongozi vichaa kama hawa wasiojali sheria zetu hadi lini?Samia ameshindwa hadi kupambana na bei ya mafuta ya kula halafu ghafla anawatangazia Watanzania kuwa yupo hadi 2030?
Sasa kama yupo hadi 2030 kama anavyodai kwa nini Serikali ijisumbue kutenga fedha nyingi kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2025?
View attachment 2159514