Rais Samia unakwama wapi kuona ubabe haufai kwenye demokrasia kama ambavyo hauifai kwenye kukusanya kodi?

Hivi majuzi mheshimiwa rais Samia amewataka maafisa wa TRA kuacha ubabe wanapofuatilia kodi kwa wananchi. Ni jambo jema.

Lakini nashindwa kuelewa kwanini rais Samia haoni pia si vizuri kutumia ubabe kuzuia maandamano ya amani ya vyama vya siasa?
Hata demokrasia alianza vizuri na 4R, akaruhusu maandamano, akaruhusu mikutano ya vyama. Pia akafuta makesi ya kubambikiza kwa wapinzani. Akawarudishia fedha wafanyabiashara zilizonyang'anywa na Magufuli. Akaenda mbali hadi kuwarudisha wakimbizi waliokuwa Ulaya akina Lissu na Lema.

Lakini CHADEMA hawakumuunga mkono. Wakaendeleza matusi, dharau kwa Rais. Walisahau kuwa uRais ni TAASISI.

Mwishowe wakaandaa maandamano ya #Samia Must Go, ndipo TAASISI ikiwapapasa kidogo kuwakumbusha wasicheze na Dola
 
Maridhiano ya 4R yalikuwa usanii maana hata suala la jaribio la kumuuwa Lissu hakuna uchunguzi uliofanyika na culprits bado ni watu wake.

Hilo ndo limechochea yaliyotokea hadi kupelekea utekaji, mateso na mauwaji ya kisiasa.

Mfano issue ya Lissu, hata mataifa makubwa yanafahamu kuwa serikali ilihusika na hata Makonda alipigwa ban kuingia marekani yeye na mke wake. Wengi tukawa tu najiuliza no haki za watu gani haswa za kuishi ambazo Makonda aliwanyima? Maana naikumbuka ile kauli ya Mike Pompeo kama vile ni jana tu.

Ina maana behind the scenes, hao wakulungwa wanaofahamu mambo ya nchi yetu kuliko wengi wetu sisi, wameona kwamba hakuna mabadiliko yoyote ukilinganisha na mwendazake aliyepachikwa udikteta.
 
Shida ni ufahamu finyu mnafikiri rais hapaswi kukosolewa hata kwenye demokrasia ya vyama vingi. Watanzania viwango vyenu ni vya chini mno ndio maana Magufuli aliamua awaburuze tu kwani hamjitambui vizuri.
 
Maridhiano ya 4R yalikuwa usanii maana hata suala la jaribio la kumuuwa Lissu hakuna uchunguzi uliofanyika na culprits bado ni watu wake.

Hilo ndo limechochea yaliyotokea hadi kupelekea utekaji, mateso na mauwaji ya kisiasa.

Mfano issue ya Lissu, hata mataifa makubwa yanafahamu kuwa serikali ilihusika na hata Makonda alipigwa ban kuingia marekani yeye na mke wake. Wengi tukawa tu najiuliza no haki za watu gani haswa za kuishi ambazo Makonda aliwanyima? Maana naikumbuka ile kauli ya Mike Pompeo kama vile ni jana tu.

Ina maana behind the scenes, hao wakulungwa wanaofahamu mambo ya nchi yetu kuliko wengi wetu sisi, wameona kwamba hakuna mabadiliko yoyote ukilinganisha na mwendazake aliyepachikwa udikteta.
Watanzania wengi hawajitambui wakisha beti basi.
 
Hivi majuzi mheshimiwa rais Samia amewataka maafisa wa TRA kuacha ubabe wanapofuatilia kodi kwa wananchi. Ni jambo jema.

Lakini nashindwa kuelewa kwanini rais Samia haoni pia si vizuri kutumia ubabe kuzuia maandamano ya amani ya vyama vya siasa?
Kodi haitishii cheo chake, weka mbali na wananchi.
 
Wahenga wanasema nyani haoni kund..lake.yeye analaumu TRA kutumia nguvu wakati yeye anateka na kuuwa.Bora anayetumia nguvu lakini haui kuliko liuwaji la watu.Halifai kabisa kukalia ofisi ya umma.2025 linatakiwa lipelekwe ICC likafungwe
 
Hata demokrasia alianza vizuri na 4R, akaruhusu maandamano, akaruhusu mikutano ya vyama. Pia akafuta makesi ya kubambikiza kwa wapinzani. Akawarudishia fedha wafanyabiashara zilizonyang'anywa na Magufuli. Akaenda mbali hadi kuwarudisha wakimbizi waliokuwa Ulaya akina Lissu na Lema.

Lakini CHADEMA hawakumuunga mkono. Wakaendeleza matusi, dharau kwa Rais. Walisahau kuwa uRais ni TAASISI.

Mwishowe wakaandaa maandamano ya #Samia Must Go, ndipo TAASISI ikiwapapasa kidogo kuwakumbusha wasicheze na Dola
Umemjibu vizuri kabisa huyo nyumbu.
 
Maridhiano ya 4R yalikuwa usanii maana hata suala la jaribio la kumuuwa Lissu hakuna uchunguzi uliofanyika na culprits bado ni watu wake.

Hilo ndo limechochea yaliyotokea hadi kupelekea utekaji, mateso na mauwaji ya kisiasa.

Mfano issue ya Lissu, hata mataifa makubwa yanafahamu kuwa serikali ilihusika na hata Makonda alipigwa ban kuingia marekani yeye na mke wake. Wengi tukawa tu najiuliza no haki za watu gani haswa za kuishi ambazo Makonda aliwanyima? Maana naikumbuka ile kauli ya Mike Pompeo kama vile ni jana tu.

Ina maana behind the scenes, hao wakulungwa wanaofahamu mambo ya nchi yetu kuliko wengi wetu sisi, wameona kwamba hakuna mabadiliko yoyote ukilinganisha na mwendazake aliyepachikwa udikteta.
Huwezi kuita usanii wakati akina Lissu wenyewe ndiyo wamekosa subira na kuanza kumporomoshea matusi Rais. Mtu kakutembelea hospitali Ubelgiji, kakuambia nini kifanyike ili urudi nyumbani. Kisha Lissu kaweka mlolongo wa mahitaji kama mafao yake ya ubunge, kufutiwa kesi za kubanbikizwa, hela ya matibabu nk.

Mama Samia kaaanza kutekeleza machache, na akiwa anatekeleza Lissu akipanda kwenye majukwaa ndiyo wa kwanza kumchafua mama kwa matusi!! Sasa mtu kama huyu unaendeleaje kumsaidia? Unaanzaje kuchunguza wauaji wake wakati mwenyewe anakudharau??
 
Wapinzani wanajifanya watoto wa mwisho, kila kitu wao ni kudeka tu.
 
Huwezi kuita usanii wakati akina Lissu wenyewe ndiyo wamekosa subira na kuanza kumporomoshea matusi Rais. Mtu kakutembelea hospitali Ubelgiji, kakuambia nini kifanyike ili urudi nyumbani. Kisha Lissu kaweka mlolongo wa mahitaji kama mafao yake ya ubunge, kufutiwa kesi za kubanbikizwa, hela ya matibabu nk.

Mama Samia kaaanza kutekeleza machache, na akiwa anatekeleza Lissu akipanda kwenye majukwaa ndiyo wa kwanza kumchafua mama kwa matusi!! Sasa mtu kama huyu unaendeleaje kumsaidia? Unaanzaje kuchunguza wauaji wake wakati mwenyewe anakudharau??
Matusi gani Lissu aliyemtukana Rais ?
 
Siku zoote wanaotetea taasisi ya Raisi ndiyo wanufaika, siyo kwamba hawajui. Ukiwa kiongozi kukosolewa NI kawaida, labda kama hujiamini au Unamaslahi binafsi
 
Matusi gani Lissu aliyemtukana Rais ?
Hata nikitaandika hapa bado utabisha. Lakini kama wewe ni mtu makini na umekuwa ukimfuatilia Lissu utagundua kuwa kauli zake ni chafu tu. Ndiyo maana hata yule Magufuli aliamua kumshambulia kwa risasi baada ya kumwita dikteta uchwara
 
Hata demokrasia alianza vizuri na 4R, akaruhusu maandamano, akaruhusu mikutano ya vyama. Pia akafuta makesi ya kubambikiza kwa wapinzani. Akawarudishia fedha wafanyabiashara zilizonyang'anywa na Magufuli. Akaenda mbali hadi kuwarudisha wakimbizi waliokuwa Ulaya akina Lissu na Lema.

Lakini CHADEMA hawakumuunga mkono. Wakaendeleza matusi, dharau kwa Rais. Walisahau kuwa uRais ni TAASISI.

Mwishowe wakaandaa maandamano ya #Samia Must Go, ndipo TAASISI ikiwapapasa kidogo kuwakumbusha wasicheze na Dola
Kwani ni lazima CHADEMA wamuunge mkono rais?

Unaelewa hayo maandamano yote ni haki ya kikatiba na kiutu?
 
Hata nikitaandika hapa bado utabisha. Lakini kama wewe ni mtu makini na umekuwa ukimfuatilia Lissu utagundua kuwa kauli zake ni chafu tu. Ndiyo maana hata yule Magufuli aliamua kumshambulia kwa risasi baada ya kumwita dikteta uchwara
Kauli chafu zipi hizo ?....kwa hiyo hilo neno 'dikteta Uchwara' lilikuwa chanzo cha Lissu kupigwa risasi?
 
Kwani ni lazima CHADEMA wamuunge mkono rais?

Unaelewa hayo maandamano yote ni haki ya kikatiba na kiutu?
Kama ni haki kikatiba mbona Magufuli aliwakatalia na hawakufurukuta??
 
This is a logical non sequitur fallacy.

Magufuli kuwakatalia na wao kutofurukuta (si kweli kwamba hawakufurukuta, watu walipinga) hakufanyi haki ya katiba kutokuwa haki ya katiba.

In fact, Magufuli kuwakatalia haki yao ya kikatiba na wao kutofurukuta siku zike ni sababu nzuri sana ya wao kutorudia kosa hilo hilo la kutofurukuta mara nyingine.

Ukikosea mara moja, hiyo si sababu ya kurudia kukosea nara nyingine.

Hiyo ni sababu ya kujizatiti usikosee mara nyingine.

Umetoa sababu kwa nini ni muhimu CHADEMA kukataa kurudi tena kwenye siasa kama za kipindi cha Magufuli.
 
Back
Top Bottom