Rais Samia unaona sahihi mechi za soka za timu za taifa kuoneshwa kwenye channels za kulipia, uzalendo uko wapi?

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
10,904
Reaction score
26,184
Ila wabongo mna nongwaaa nyie..!
 
Katika jambo ambalo wizara ya michezo wanatukosea ni hili....

Kimsingi mechi zote zinazoihusu Timu ya Taifa zinapaswa kuonyeshwa Moja kwa Moja kupitia Televisheni ya Taifa...tena Bure kabisa...

Sasa sijui viongozi wa Wizara husika wanafanya Nini?
 

Zinatakiwa hela. Ng'ombe shuruti akamuliwe hadi damu!

Lucas Mwashambwa, Tlaatlaah, Uhakika Bro, mama anatosha, 5 mingine.
 
Zinatakiwa hela. Ng'ombe shuruti akamuliwe hadi damu!

Lucas Mwashambwa, Tlaatlaah, Uhakika Bro, mama anatosha, 5 mingine.
Ndiyo,
Dr.Samia Suluhu Hassan, kipenzi cha waTanzania mi5 tena ikulu bila mbambamba yoyote..

Na kama kawaida kama dawa, ataendelea kutoa zawadi ya mamilioni kwa goli la mama kwa mechi zote za kimataifa kwa vilabu vyetu nchini vinavyoshiriki mashindano ya kimataifa, Lakini zaidi sana mechi za timu ya Taifa zitakua live kupitia vituo vya utangazaji vya umma hususani tbc Taifa πŸ’

nchi nyingine ulizozitaja hazituhusu chochote kwenye masuala yetu ya ndani, na by the way hakuna cha kuiga wala kujifunza kutoka kwao hata kimoja kwasababu hawana furaha ni watu wa fujo tu, ulitaka watulizwe na nini gentleman?

Tanzania itaendelea kua nchi ya umoja, amani na utulivu daima bila kujali mihemko ya mtu yeyote moja, anaelalamikia na kufananisha mambo ya Tanzania na ya huko kwenye vurugu kila uchwao, hiyo ni useless πŸ’
 

Ungekuwa umemtendea fadhila zaidi kumjibia kama majibu unayo.

Wana nzengo wanauliza:

"Rais Samia unaona sahihi mechi za soka za timu za taifa kuoneshwa kwenye channels za kulipia, uzalendo uko wapi?"

Kwenye bandiko lako, majibu yao yamo?
 
Ungekuwa umemtendea fadhila zaidi kumjibia kama majibu unayo.

Wana nzengi wanauliza:

"Rais Samia unaona sahihi mechi za soka za timu za taifa kuoneshwa kwenye channels za kulipia, uzalendo uko wapi?"

Kwenye bandiko lako, majibu yao yamo?
zingatia ukweli wa maelezo muhimu,

Kama Taifa ni lazima kua wazalendo hasa kwenye suala la kulipa kodi, hakuna haja kujificha kwenye mechi live , ambazo ukifungulia vituo vya habari vingi tu achilia mbali vya umma viko live na ni Free...

Hata hivyo,
Vipaumbele vya waTanzania ni pamoja na maji, afya, elimu, miundombinu, kilimo, biashara, ufugaji, uvuvi n.k na si vinginevyo gentleman πŸ’
 
Nenda banda umiza 500 kazi kuonga mademu tu. Kutoa 500 banda umiza hautaki na kutwa kusifia mama anapiga mwingi mbuzi kagoma weww.
 

Wana nzengo wanataka majibu yao, nje ya hapo yote uliyoandika ni ugoro kama mwingine tu ndugu.
 
Wana nzengo wanataka majibu yao, nje ya hapo yote uliyoandika ni ugoro kama mwingine tu ndugu.
TBC mechi ya Taifa Stars walikua live na vyombo vingine vingi tu nchini pia walikua live hicho cha kufananisha na huko kwa watu wa fujo na vurugu mie ndiko hasa ningependelea kupaelezea...

vinginevyo,
mengine ni malalamiko yasiyo na tija kwa vitu bayana πŸ’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…