Rais Samia, unapoteua zingatia watumishi wa muda mrefu na wenye uzoefu serikalini badala ya kuwatoa mtaani

Hapa suluhisho ni Katiba Mpya tu ya Wananchi. Hivi vyeo vyote vya kipuuzi tuliviondoa. Maana vinaongeza tu matumizi serikalini huku vikiwa havina tija yoyote ile.
 
Ushauri wake Ni mzuri,

Lakini haujakamilika kwa asilimia zote,

Pia hata mapendezekezo yako wewe pia Ni mazuri

Hivyo katika ushauri wake na nyongeza yako

Kwa pamoja tunapata mawazo mazuri ambayo kama yakifanyiwa kazi

Ni faida kwa nchi
 
Sawa, lakini wawe na angalau mwelekeo mwema katika jamii.
Hilo ni swala lingine kaka. Kawaida cheo kinamshepu mtu.., bila shaka kama kuna ambao hawana mwelekeo mwema watabadilika kutokana na majukumu.
 
Nina rafiki yangu anasoma sheria huwa tunamdiss mwanasheria gani unavaa mnyonyo, crazy jeans na buti la jeje. Kuanzia jana anatuponda vibaya anatuonesha picha za Nikk wa pili akiwa kavaa pensi, Air Force mguuni sunglasses na cheni uku amekaa kwenye meza inazungukwa na vinywaji. Anatwambia kama huyu kama DC, mi nani mpaka nivae bwanga. Alafu tukawa na playlist yake nyimbo kama Mpubu na Arosto
 
Binafsi sijawahi sikia background ya Nikki ndo mana nikauliza ikoje. Hongera zake bwashee
 
Mleta mada uko sahihi kwa 100%.
Hivyo ndivyo ilipaswa kuwa na inapaswa kuwa. Mtumishi mwandamizi wa umma ndio anapaswa kupandishwa na kuwa DAS, DED, DC, RC nk. Kuokoteza watu mitaani ni jambo la ovyo kabisa.
 
Hilo la Kalist kupewa cheo ninalipinga kwa 100%. Kwanini? Kalist anapewa cheo sasa kama fadhila za kuunga mkono juhudi na sio kwa sababu ya utendaji wake kama meya wa Arusha. Kile kitendo kiliharibu mwenendo mzima wa utendaji wake, hapaswi kupewa cheo. Tukiendelea na hizi tabia tutaishia kuwa na nchi ya kinafiki sana.
 
Naunga mkono hoja
 
Hakuna Rais hapo nchi ipo ipo tu Mungu atusaidie Watanzania.
Punguani wewe unasumbuliwa na roho mbaya na husda unataka amtue baba yako ndiyo uone raha, na bado mtaumia sana.
 
Sekta binafsi hamna watu wenye uwezo mpaka watoke serikalini?
 
Ni muhimu sifa za msingi na taratibu zikafuatwa hatua kwa hatua kabla ya mtu kutoka sekta binafsi kupewa nafasi za juu serikalini.
Hizi logic tujiulize.....
1. Ni sekta ipi mhusika amekuwepo? (Yaani mtu ni mtangazi wa Redio au Tv binafsi halafu ghafla anapewa ukuu wa wilaya, logic iko wapi? )

2. Amekuwa akifanya kazi eneo lipi? (Yaani mtu anaishi na kufanya kazi sekta binafsi jijini Dar, ghafla anateuliwa mkuu wa wilaya ya Maswa huko Shinyanga, logic iko wapi?)

3. Hivi mhusika ni lazima apewe vyeo vya kiutawala kama DC, DED, DAS, RAS, RC? (Kwanini mtangazi wa redio au Tv asipewe uhafisa habari wa taasisi ya serikali kwanza, akaingia kwanza mifumo ya utendaji wa serikali, akafunga ndoa ya kiutumishi na serikali, halafu ikibidi na kupendeza huko baadaye ndio akapewa cheo cha kiutawala)
 
Hoja yako number tatu nimeikubali kabisa, ila kutoka sector binafsi watu hufanya different positions Hadi za kiutawala, Kuna wanaotokea kwenye organization na wazoefu wazuri wanaweza kuja na something new.
Kwa nilichokiona watumishi wengi wa serikali huwa Wana mazoea ya kazi na hawafikirii nje ya box tofauti na waliotoka sector binafsi au kwenye organization za kimataifa utendaji huwa tofauti na wanayo mengi ambayo watumishi hawajui.
So ni Bora kuwa na integration system ya kupata watu competency kwenye nafasi mbalimbali na wazoefu sio ki base kwa watumishi eti 20 year's mtu Yuko wilayani Hana experience hata ndogo ya kimataifa utegemee positive change never on earth.
Mama achaganye tu kuleta ufanisi
 
Sekta binafsi hamna watu wenye uwezo mpaka watoke serikalini?
Embu waza tu.
Miaka kumi iliyopita mtu alimaliza chuo na wenzake kadhaa, akaomba ajira serikalini ya ualimu, akapata ajira ya kuwa mwalimu huko wilaya ya Namtumbo kijiji kimoja ndani ndani, kwa kuwa mazingira ni magumu na mshahara ni mdogo akaona ni bora aende sekta binafsi jijini Dar lakini wenzake wakaenda kufanya kazi hivyo hivyo, yeye akabakia jijini akapata umaarufu mkubwa, akajulikana na wakuu, leo anateuliwa kuwa DC.

Sasa, tuanze kujiuliza haya maswali.
1. Nini mantiki ya kuitumikia Jamhuri kwa muda mrefu halafu inapofika kupewa vyeo vya juu kusiwe na mantiki?

2. Nini mantiki ya uzoefu kwenye utumishi wa umma, ikiwa umaarufu wa kijamii unatosha kuwepo vyeo vya juu?

3. Kwanini mtu kutoka sekta binafsi asipimwe kwanza uwajibikaji wake kwa umma kwa kufanya kazi katika ngazi ya chini kabla ya kupewa cheo cha juu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…