Rais Samia, unapoteua zingatia watumishi wa muda mrefu na wenye uzoefu serikalini badala ya kuwatoa mtaani

Embu waza tu.
Miaka kumi iliyopita mtu alimaliza chuo na wenzake kadhaa, akaomba ajira serikalini ya ualimu, akapata ajira ya kuwa mwalimu huko wilaya ya Namtumbo kijiji kimoja ndani ndani, kwa kuwa mazingira ni magumu na mshahara ni mdogo akaona ni bora aende sekta binafsi jijini Dar lakini wenzake wakaenda kufanya kazi hivyo hivyo, yeye akabakia jijini akapata umaarufu mkubwa, akajulikana na wakuu, leo anateuliwa kuwa DC.

Sasa, tuanze kujiuliza haya maswali.
1. Nini mantiki ya kuitumikia Jamhuri kwa muda mrefu halafu inapofika kupewa vyeo vya juu kusiwe na mantiki?

2. Nini mantiki ya uzoefu kwenye utumishi wa umma, ikiwa umaarufu wa kijamii unatosha kuwepo vyeo vya juu?

3. Kwanini mtu kutoka sekta binafsi asipimwe kwanza uwajibikaji wake kwa umma kwa kufanya kazi katika ngazi ya chini kabla ya kupewa cheo cha juu?
Kwa katiba unasemaje kuhusu cheo cha DC?
 
Naunga mkono maandishi yako,

Teuzi hizi zinaua uzalendo kazini na kwa watumishi. Mtu hajawahi kuhudumu serikalini,ghafla anapewa UDC. Hakuna mfumo mzuri wa kupata watu hawa,ni nafasi zimekaa kiupigaji na za kupeana shukràni.

Bora zifutwe tu.
 
Hakuna Rais hapo nchi ipo ipo tu Mungu atusaidie Watanzania.
🤣🤣 Mkuu Hakuna ulazima wa Rais kukuteua wewe.....

Unarudiarudia maneno kila THREAD inayobandikwa JF ha ha ha

UTEUZI nchi hii hajauanza mh.Rais Samia......

#KAZIIENDELEE
 
Naunga mkono maandishi yako,

Teuzi hizi zinaua uzalendo kazini na kwa watumishi. Mtu hajawahi kuhudumu serikalini,ghafla anapewa UDC. Hakuna mfumo mzuri wa kupata watu hawa,ni nafasi zimekaa kiupigaji na za kupeana shukràni.

Bora zifutwe tu.
Mkuu hivi kila mtumishi wa UMMA ni mwanaCCM ?!!!

Tusisahau kuwa unapoteuliwa uDC unakuwa pia mjumbe wa kamati ya siasa wilayani.....

#KaziIendelee
 
Ninashauri ni wakati wa serikali kufikiria namna nzuri kufanya teuzi mbalimbali katika nafasi za serikali kwa kuzingatia uzoefu wa Kazi serikalini ,uadilifu ili kutengeneza uzalendo .

kwa mfano haileti taswira nzuri kumuacha katibu wa tarafa au maafisa wameoshika nyadhifa mbalimbali ktk Idara zao wilayani au mikoani aliekaa kazini miaka 15 na zaidi serikalini mwenye elimu ya kutosha wengine wanawazidi hata elimu Ma DC ma Das na Ma RC lkn ukapuuza utumishi wao ukatoa watu mtaani kuja kuwa Ma DC, DAS,RC’s ,RAS etc .

Zamani Kila mfanyakazi alijua iwapo atahudumu kwa mda mrefu na uadilifu angefika katika nafasi ya juu kwa bidii yake ya Kazi uadilifu na kujituma ,na hiyo ndio kulikozaa uzalendo hapo zamani ma Afisa utumishi, makatibu tarafa, maafisa maendeleo , kilimo , Afya,Walimu, walipanda nafasi za juu za kiselikali na hiyo ilijenga kuwa na viongozi wengi wenye uadilifu uzalendo na kupenda nchi sbb walipanda nafasi kwa mafaili yao na si kwa majina yao.

Maafisa wakuu wa idara mbalimbali kutoka sekta tofauti mfano elimu, Afya, kilimo, maendelo, utawala iwe wilayani au mkoani wenye miaka 20 ktk kazi ,uzoefu na weledi serikalini ndoto zao nao ni kushika nafasi za juu ktk wilaya au mkoa unapowaletea mtu ambae hajawahi kuwa mtumishi huwaongezei tija ila unawavunja moyo na hiyo inashusha uzalendo wa nchi na tija kwenye Kazi zao, Hawa walitegemea miongoni mwao ndio atakaepanda na huo ndio utaratibu wa huko nyuma.

mfumo huu uangaliwe upya kwa nini mfano makatibu tarafa na maafisa wengine wa wilaya wasipande kuwa Ma DAS na ma DC na wakurugenzi wa halmashauri halafu hao wapya nao wakaanzia chini kupata uzoefu na kupimwa huko chini na kujifunza kujua mifumo ya serikali inafanyaje Kazi kuanzia chini . Huko nyuma hatukuwahi kuona Ma DC ma Ma RC wakivunja maadili sbb walitokana na mfumo mzuri vyeo havikuwapa ukichaa kwani walipanda navyo polepole, hivyo waliheshimu sana utu na maadili ya Kazi na miiko ya kazi zao.

Zamani watu waioshika nafasi hizo Walionekana ni watu wenye heshima iliotukuka na wazalendo kweli kweli na Jamii ziliwaheshimu sana ila leo Jamii inaziona nafasi hizo kama ni zakupewa kwa wateule fulani waliokosa fursa mahali pengine .

Na shauri serikali ianze marekebisho kwa Kurekebisha hili kwenye mkeka wa MA DAS iwapo kutakuwa na mabadiliko kwenye nafasi hizo.
Upo sahihi kabisa. Nafikir toka awamu ya nne, tano na hii ya Sita kumekuwa na teuzi za hovyo hovyo za kupeana bila ya kuzingatia weredi wa wateule. Huko kwenye halmashaur kumekuwa na lugha gongana Kati ya wakurungez, wakuu wa idara na madc kwenye maamuz. Utakuta DCs, RCs Hana exposure na masuala ya utumishi wa umma, analazimisha mkurugenz kukiuka taratibu.
 
Kuna sehemu Wanasema anasoma PhD ya development studies
Msomi huyo....ana zaidi ya shahada 2.....

Ila hata Kama angekuwa ni FORM 6 LEAVER....ila jamaa yuko SMART UPSTAIRS......

#KaziInaendelea
#NchiKwanza
 
Apo utaambiwa acha na wenyewe wapate ajira
 
Mkuu hivi kila mtumishi wa UMMA ni mwanaCCM ?!!!

Tusisahau kuwa unapoteuliwa uDC unakuwa pia mjumbe wa kamati ya siasa wilayani.....

#KaziIendelee
Basi hawa watu watafutwe kwa utaratibu maalumu sio kama hivi ni kama vya kupeana.
 
Upo sahihi kabisa. Nafikir toka awamu ya nne, tano na hii ya Sita kumekuwa na teuzi za hovyo hovyo za kupeana bila ya kuzingatia weredi wa wateule. Huko kwenye halmashaur kumekuwa na lugha gongana Kati ya wakurungez, wakuu wa idara na madc kwenye maamuz. Utakuta DCs, RCs Hana exposure na masuala ya utumishi wa umma, analazimisha mkurugenz kukiuka taratibu.
Ulikuwepo kipindi cha awamu za mwanzo?!!

Una uhakika kila ulichohadithiwa na kusifiwa kuwa hakukuwa na makosa kwenye vetting ni Kweli ?!!!

Kazi ya CHAMA CHA SIASA ni kushika na kuiendeleza hatamu....

Sioni makosa kwa WALIOTEULIWA kwani wanakwenda KUISAIDIA serikali ya CCM kututumikia WATANZANIA......

#KaziIendelee
#NchiKwanza
 
Mkuu hivi kila mtumishi wa UMMA ni mwanaCCM ?!!!

Tusisahau kuwa unapoteuliwa uDC unakuwa pia mjumbe wa kamati ya siasa wilayani.....

#KaziIendelee
Mimi naamin wilaya zina watu wanaoweza shika hizo nafasi.
 
Hapana..! Kuchanganya ndio njia bora. Hao watendaji wa serikali unaowasema wawepo, na hao wa mtaani pia wawepo, wa private sector wawepo, wa vyama pinzani wawepo, wa jumuiya na asasi za kiraia pia wawepo, nk. Hapo ndipo tutajenga taifa lenye umoja na mshikamano..
Umoja upi mkuu!??kwani kwa katiba hii hakuna mpinzani, wala mwanaharakati/mtu kutoka jumuia na asasi za kiraia anayeweza kuteuliwa kuwa DC, RC, akabakia kuwa sio mwana CCM, kwani lazima anaenda kuwa muuzaji na msimamizi mkuu wa sera za ccm huko, na vikao vyote vya chama ataingua, hapo utasemaje tena bado atakuwa mpinzani?!!huo uteuzi wa jana kuna mtu ambaye sio mwana CCM?Watu wanapopigania katiba mpya ni kukomesha mambo haya, yaani vyeo vina kuwa ni kulipana fadhira tu.
 
Basi hawa watu watafutwe kwa utaratibu maalumu sio kama hivi ni kama vya kupeana.
Utaratibu maalum upi mkuu ?!!!

Hao ni "wanasiasa"....ni lazima uende kisiasa.....

Ndio kazi ya CHAMA tawala kushika hatamu......

Ikiwa CHADEMA wanatumia PLATFORMS za watu wa SOCIAL MEDIAS basi si kosa kwa CHAMA CHA MAPINDUZI "kuenenda" hivyo....

Dunia IMEBADILIKA...hii si miaka ile ya AZIMIO LA ARUSHA.....

Nakupata sana ndugu yangu.
 
... pangu pakavu in ACTION!
1624170127081.png
 
Kwa nini wanaofanya private sector wanataka kuhamia serikalini? Kwa nini hao wanaotoka private sekta wasianzie kuwa watendaji wa kata au watumishi wa ngazi za chini huko wilayani?
Sikubaliani na ushaur wako aisee ulisema wawe watumishi wa serikali vipi wanaofanya private sector na wako vizuri hafu unasema achukue waliokaa serikalini 20 years hao hata utendaji huwa wa mazoea Tena hawana exposure yoyote, Bora kuteua hata wa binafsi wenye exposure ili kuleta mabadiliko
 
Umeelewa alichosema mleta uzi?
Hapana..! Kuchanganya ndio njia bora. Hao watendaji wa serikali unaowasema wawepo, na hao wa mtaani pia wawepo, wa private sector wawepo, wa vyama pinzani wawepo, wa jumuiya na asasi za kiraia pia wawepo, nk. Hapo ndipo tutajenga taifa lenye umoja na mshikamano..
 
Ukishampa rais nguvu za kikatiba na kisheria za kuteua na kutengua yeyote, hutakiwi kuanza kumpangia nani wa kuteua na kutengua.

Kama vipi, unaona mfumo wa sasa haufai, badilisha katiba na sheria husika ili hivi vyeo vipatikane kwa mchakato tofauti wenye vigezo tofauti, au viondolewe kabisa.
 
Back
Top Bottom