Rais Samia, unapoteua zingatia watumishi wa muda mrefu na wenye uzoefu serikalini badala ya kuwatoa mtaani

Kwa katiba unasemaje kuhusu cheo cha DC?
 
Naunga mkono maandishi yako,

Teuzi hizi zinaua uzalendo kazini na kwa watumishi. Mtu hajawahi kuhudumu serikalini,ghafla anapewa UDC. Hakuna mfumo mzuri wa kupata watu hawa,ni nafasi zimekaa kiupigaji na za kupeana shukràni.

Bora zifutwe tu.
 
Hakuna Rais hapo nchi ipo ipo tu Mungu atusaidie Watanzania.
🤣🤣 Mkuu Hakuna ulazima wa Rais kukuteua wewe.....

Unarudiarudia maneno kila THREAD inayobandikwa JF ha ha ha

UTEUZI nchi hii hajauanza mh.Rais Samia......

#KAZIIENDELEE
 
Naunga mkono maandishi yako,

Teuzi hizi zinaua uzalendo kazini na kwa watumishi. Mtu hajawahi kuhudumu serikalini,ghafla anapewa UDC. Hakuna mfumo mzuri wa kupata watu hawa,ni nafasi zimekaa kiupigaji na za kupeana shukràni.

Bora zifutwe tu.
Mkuu hivi kila mtumishi wa UMMA ni mwanaCCM ?!!!

Tusisahau kuwa unapoteuliwa uDC unakuwa pia mjumbe wa kamati ya siasa wilayani.....

#KaziIendelee
 
Upo sahihi kabisa. Nafikir toka awamu ya nne, tano na hii ya Sita kumekuwa na teuzi za hovyo hovyo za kupeana bila ya kuzingatia weredi wa wateule. Huko kwenye halmashaur kumekuwa na lugha gongana Kati ya wakurungez, wakuu wa idara na madc kwenye maamuz. Utakuta DCs, RCs Hana exposure na masuala ya utumishi wa umma, analazimisha mkurugenz kukiuka taratibu.
 
Kuna sehemu Wanasema anasoma PhD ya development studies
Msomi huyo....ana zaidi ya shahada 2.....

Ila hata Kama angekuwa ni FORM 6 LEAVER....ila jamaa yuko SMART UPSTAIRS......

#KaziInaendelea
#NchiKwanza
 
Apo utaambiwa acha na wenyewe wapate ajira
 
Mkuu hivi kila mtumishi wa UMMA ni mwanaCCM ?!!!

Tusisahau kuwa unapoteuliwa uDC unakuwa pia mjumbe wa kamati ya siasa wilayani.....

#KaziIendelee
Basi hawa watu watafutwe kwa utaratibu maalumu sio kama hivi ni kama vya kupeana.
 
Ulikuwepo kipindi cha awamu za mwanzo?!!

Una uhakika kila ulichohadithiwa na kusifiwa kuwa hakukuwa na makosa kwenye vetting ni Kweli ?!!!

Kazi ya CHAMA CHA SIASA ni kushika na kuiendeleza hatamu....

Sioni makosa kwa WALIOTEULIWA kwani wanakwenda KUISAIDIA serikali ya CCM kututumikia WATANZANIA......

#KaziIendelee
#NchiKwanza
 
Mkuu hivi kila mtumishi wa UMMA ni mwanaCCM ?!!!

Tusisahau kuwa unapoteuliwa uDC unakuwa pia mjumbe wa kamati ya siasa wilayani.....

#KaziIendelee
Mimi naamin wilaya zina watu wanaoweza shika hizo nafasi.
 
Umoja upi mkuu!??kwani kwa katiba hii hakuna mpinzani, wala mwanaharakati/mtu kutoka jumuia na asasi za kiraia anayeweza kuteuliwa kuwa DC, RC, akabakia kuwa sio mwana CCM, kwani lazima anaenda kuwa muuzaji na msimamizi mkuu wa sera za ccm huko, na vikao vyote vya chama ataingua, hapo utasemaje tena bado atakuwa mpinzani?!!huo uteuzi wa jana kuna mtu ambaye sio mwana CCM?Watu wanapopigania katiba mpya ni kukomesha mambo haya, yaani vyeo vina kuwa ni kulipana fadhira tu.
 
Basi hawa watu watafutwe kwa utaratibu maalumu sio kama hivi ni kama vya kupeana.
Utaratibu maalum upi mkuu ?!!!

Hao ni "wanasiasa"....ni lazima uende kisiasa.....

Ndio kazi ya CHAMA tawala kushika hatamu......

Ikiwa CHADEMA wanatumia PLATFORMS za watu wa SOCIAL MEDIAS basi si kosa kwa CHAMA CHA MAPINDUZI "kuenenda" hivyo....

Dunia IMEBADILIKA...hii si miaka ile ya AZIMIO LA ARUSHA.....

#KaziInaendelea
#NchiKwanza
 
Nakupata sana ndugu yangu.
 
Kwa nini wanaofanya private sector wanataka kuhamia serikalini? Kwa nini hao wanaotoka private sekta wasianzie kuwa watendaji wa kata au watumishi wa ngazi za chini huko wilayani?
 
Umeelewa alichosema mleta uzi?
 
Ukishampa rais nguvu za kikatiba na kisheria za kuteua na kutengua yeyote, hutakiwi kuanza kumpangia nani wa kuteua na kutengua.

Kama vipi, unaona mfumo wa sasa haufai, badilisha katiba na sheria husika ili hivi vyeo vipatikane kwa mchakato tofauti wenye vigezo tofauti, au viondolewe kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…