Rais Samia, unapoteua zingatia watumishi wa muda mrefu na wenye uzoefu serikalini badala ya kuwatoa mtaani

Tatizo ni kwamba hata hao wenye maadili mema hufanya vituko vitupu. Kuna wale waliosaini mikataba wakiwa Ulaya kwa masharti ya wazungu, ukizitazama CV zao ni waheshimiwa wakubwa wenye muonekano wa hali ya juu.

Cha muhimu kwa hivi vyeo ni uzalendo wa mtu, kujituma kwa mtu, ubunifu wa mtu. Hizo personalities zimeikwaza sana Tanzania kuanzia awamu ya tatu kuja hizi za sasa. Tusipende kuyakariri haya maisha.
 
Mimi nafikiri watu wateuliwe kulingana na weledi wao kiutendaji na sio kuangalia watumishi wa umma tu. Watumishi wengi wa umma hufanya kazi kimazoea na wamejaa viburi hatari. Mtu ofisi anaifanya kama yake na kufanya vile atakavyo.
 
ACHA JAZIBA!.
Although nilisema "mfano" ila umekuja kama simba aliyejeruhiwa!.

Ila ndiyo kesha pewa hivyo anakwenda "sasa unaingia mkoa wa Mara"
 
Mama anajaribu kufuta Mwendazake mentality. Hao unaoita wenye uzoefu ndio wametufikisha hapa tulipo
 
Kuchanganya kama ulivyosema ni sawa,lakini kumchukua PHD holder unaweka kwenye rank mmoja na muigizaji wa bongo movie kwa maoni yangu sio sahihi.
 
Ushauri mzuri sana. Miaka yamwisho ya utawala wa Nyerere, nadhani zaidi ya nusu ya maDC ni watu waliowahi kuwa makatibu watendaji wa Tarafa (kuna kipindi wakiitwa Division Executive Secretary) ; na walitumia madaraka yao vizuri sana na kwa weledi wa juu sana.
 
Kuchanganya kama ulivyosema ni sawa,lakini kumchukua PHD holder unaweka kwenye rank mmoja na muigizaji wa bongo movie kwa maoni yangu sio sahihi.
Kama huyo PHD ameridhika kuna tatizo gani?
 
Kwa nini wanaofanya private sector wanataka kuhamia serikalini? Kwa nini hao wanaotoka private sekta wasianzie kuwa watendaji wa kata au watumishi wa ngazi za chini huko wilayani?
Kila mtanzania ana Uhuru wa kuteuliwa na kufanya serikalini au private, Tena wa serikalini ubunifu huwa ni zero maana wanajua ukipata kazi mpaka uzeeke nayo
 
acha ubinafsi wewe kwani walioko serikalini ndo wana uwezo zaidi ya walio kwenye private sector na NGOs? wakati walipo serikalini hata ukimwambia andika riport ya kiingereza anashindwa kabisa....
 
Kufanya kazi serikalini Ni utumwa wa Aina fulani hivi .

Thamani yako haionekani hata kidogo .

Ukifa kesho wengine watajaza hio nafasi sio wanao Wala ndugu yako ataiziba nafasi yako.

Kuna watu wanafanya kazi Wana masters ,post graduate Ila wapi wanapokea mishahara ya laki laki Hadi Leo hawana marupurupu yeyote .

Mi naona kufanya kazi serikalini iwe Target tu uki hit target unatoka unafanya harakati zingine
 
Sawa la exposure Ni niambie mtu Kama chopa mchopanga ana exposure gani kwenye Mambo ya serikali .

Kwenye taratibu za uendeshaji wa kazi za kiserikali anajua Nini ?

Exposure unayoiongelea hapa Ni ipi !? Ile kusafiri nje ya nchi au ipi?

Kumchagua DC,RC,auDED kutoka Kita Ni sawa na kuwapeleke wanajeshi general ambaye hajui hata kufanya usafi wa silaha kwa kuzingatia Sheria za usalama wa silaha .

Otherwise utakuwa una faidika na hizi teuzi
 
Sasa huyo mchopanga namjua kwenye bongo movie tu ila Kuna watu wengi wazuri wazoefu na wenye exposure hawako serikalini huko na hawajaingia siasani na ni watendaji wazuri kuliko huko serikalini na wenye maono na hawajapata nafasi. So nafasi zikianza kutolewa kwa utendaji mbona wapo wengi.
 
Ushauri huu ni mzuri mno pia utapunguza wanasiasa uchwara hasa wa chama tawala wanaoishi kwa kuvizia teuzi kila kukicha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…