Accumen Mo
JF-Expert Member
- May 15, 2022
- 18,036
- 39,882
Wasalaam wanajf
Kama kichwa mada hapo, hili suala linasikitisha sana kwa kweli nimeona nitoe ya moyoni juu yanayoendelea, inasikitisha sana pale ambapo tunaona Rais anafumua mifumo ya mtangulizi wake bila ya kujua uhalisia wa mambo hayo.
Pia nikupongeze kwa kumteua Bw. Lyimo kuwa kamishina wa kudhibiti madawa ya kulevya, huyu ni mtu sahihi kwa wakati sahihi wengi tunamjua na kazi yake inaonekana. Pia, muongezee ulinzi wa kutosha ni mtu anayepambana na genge la majambazi wa nchi.
Baadhi ya mifumo iliwekwa madhubuti ili kuzuia wizi ila Rais wetu unafumua tu bila ya kuangalia mara mbili , hii ni kutokana na ushauri kutoka kwa watu wako wa karibu ..Kwanza lazima ukubali kama Rais hauwezi kujua kila na uendeshaji wake, mbaya zaidi unategemea washauri ambao kiuhalisia wanakupotosha.
Miongoni mwa mifumo aliyoweka mtangulizi wako ni malipo ya control number , bidhaa muhimu kama madini , nyara serikali (Government trophies) , Mafuta na gasi yaani bidhaa muhimu nchi ziwe zinaondoshwa na kuingia chini ya uangalizi wa wakala serikali ila mlikuja mkavunja huo mfumo bila ya kujua aliyeweka alikuwa na maana gani.
Nchi maskini kama hii unawezaje kuacha madini yasafirishwe na watu binafsi , watu wanaondosha shehena ya madini pale bandari kwa kudanganya thamani halisi ya madini inakuwa chini(under declared customs svalue) hapo serikali inakosa mapato halisi ya thamani ya madini . Tunasikia watu wanatorosha kwenda kenya je , ni kwa namna gani unaacha watu binafsi wanapitisha mpakani bila ya serikali kujua? Wakati huko nyuma mtangulizi wako alikuwa na mfumo mzuri ila wewe ulikuja kudanganywa ukautoa.
Nchi haiwezi kuendelea ikiendeshwa kama timu ya mpira, kila mtu anakuja na mifumo yake ila ukizingatia hata wewe Rais ulikuwe ni sehemu ya mtangulizi.