Bosi usisumbuke, mimi nina nadharia ya kijinga kijinga. Dkt Samia kama mwenzake Dkt Magufuli, tofauti ni kuwa Dkt Magufuli nadhani aliamini ktk ushauri wa TISS na alifanyia kazi report na mapendekezo ya TISS, Dkt Samia nadhani akipelekewa yeye huwa anakuwa na washauri wengine ambao hawampendi maana wanajiona wao ndiyo walimuweka na kumfikisha hapo alipo na hivyo wanahakikisha hafanyi maamuzi sahihi, na inamgharimu urais wake na mpaka sasa chuki kuu imesababishwa na hilo genge ambalo anadhani ni zaidi ya mfumo halisi. Mama yetu, Dkt Samia kazi iliyopo mbele yake ni ngumu sana, ingawa kikundi fulani anashani ndiyo sahihi zaidi na kimekuwa kikimdanganya bila yeye kuona uhalisia. Mfano tu chuki iliyopo kwa wapiga kura ni kubwa sana tena sana ila akina Mchengerwa ndiyo kawaamini hahaha wakimuambia Mama unaupiga mwingi basi anadhani ni kweli. Kwa ujumla tumuombee Dkt Samia maana kama hatopita kama rais 2025 basi inawezekana kama taifa tukawa na hali ngumu sana mbeleni kwa sababu huyo atakayekuja atataka kufumua mifumo yote ya kifisadi ya Dkt Samia na akiwa anafanya hivyo maana yake nchi haitapiga hatua ni kama yeye Dkt Samia alivyofumua ya Dkt Magufuli matokeo yake miaka yake ya urais ameitumia kufumua ya Dkt Magufuli na kujaribu kuonesha yeye ni better kuliko Dkt Magufuli kitu ambacho kimemgharimu sana na kumshushia hadhi yake mbele ya wapiga kura. So ni bora Dkt Samia aendelee ili tuwe na stability ya uchumi angalau mpaka 2030.